Watu 29 Wapoteza Maisha Katika Ajali Mkoani Singida

9ded1fe1-3cb5-46f7-b0a1-f4533dbf4018

Ajali mbaya imeyohusisha mabasi mawili ya kampuni ya City
Boy imetokea katika kijiji cha Maweni wilaya ya Manyoni,
Singida na kusababisha watu 29kupoteza maisha papo hapo
huku chanzo cha ajali kikitajwa kuwa ni mwendo kasi.

Mabasi hayo yenye namba za usajili T531 DCE na T247 DCD,
moja lilikuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Kahama na
lingine likitokea Kahama kuelekea Dar es Salaam.

Moja ya mashuhuda wa ajali hiyo amesema kuwa
madereva wa mabasi yote walikuwa katika mwendo kasi na
wakati ajali inatokea walikuwa wakisalimiana kwa kunyosheana
mikono kisha basi moja kupoteza mwelekeo na kuingia upande
wa basi lingine na ndipo yakakutana uso kwa uso na kusababisha
ajali hiyo.

Kamanda wa Polisi Singida, Thobias Sedoyeka tayari
amethibittisha kutokea ajali hiyo na uchunguzi zaidi unaendelea
kufanyika.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli ametuma salamu za
rambirambi na kueleza kuwa amepokea taarifa hiyo kwa mshtuko
na amesikitishwa na ajali hiyo ambayo imechukua maisha ya
watanzania.