Kivuko cha Mto Kilombero Mkoani Morogoro Kimezama kikiwa na abiria zaidi ya 30 na magari matatu.
Mkuu wa wilaya ya Kilombero , Bw Leph Gembe ametibitisha kutokea kwa tukio hilo jana usiku majira ya saa moja wakati kivuko hicho kikielekea Ulanga.
Amesma kuwa jumla ya watu zaidi ya 30 walikuwe katika kuvuko hicho na kuwa jitihada za uokoaji zilifanyika na zaidi ya watu 29 waliokolewa katika tukio hilo.
Aliongeza kuwa chanzo ch ajiali hiyo ni kuwepo kwa upepo mkali na mawimbi yaliyopelekea kivuko hicho kuzama, hivyo alisisitiza kuwa ataendelea kutoa taarifa kulingana na matukio yanayojitokeza katika eneo hilo
Hata hivyo leo mapema Huko bungeni Dodoma Kwenye taarifa hiyo Waziri Jenista Mhagama amesema watu 30 wameokolewa kati ya watu 31, jitihada zinaendelea kuokoa watu pamoja na mali. Picha na issamichuzi.blogspot.com