Mwanzilishi wa Mfuko wa Starkey Hearing, William Austin (kulia) akisaidiana na Mkewe Tani Austin (kushoto) kumvalisha kifaa cha kumwezesha kusikia mtoto Malechela Juma (katikati) leo jijini Dar es Salaam wakati mfuko huo ulipoendesha huduma ya kutoa vifaa vya kusaidia kusikia kwa watu wenye matatizo ya kusikia ambayo itatolewa kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam zaidi 2000 kwa muda wa siku nne katika Hoteli ya Serena.
Baadhi ya wakazi na watoto kutoka sehemu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam wakiwa katika foleni ya kupatiwa matibabu ya huduma ya vifaa vya kuwasaidia kusikia kutoka Mfuko wa Starkey Hearing leo jijini Dar es Salaam. Mfuko huo umeweka kambi katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo wanatarajia kutoa huduma hiyo bure kwa watu zaidi ya 2000 kwa kipindi cha nne.
Mwanzilishi wa Mfuko wa Starkey Hearing William Austin (kulia) akisaidiana na Mkewe Tani Austin (kushoto) kumuvalisha kifaa cha kumwezesha kusikia mtoto Lilian Vincent (leo) jijini Dar es Salaam wakati Mfuko huo ulipoendesha huduma ya kutoa vifaa vya kusaidia kusikia kwa watu wenye matatizo ya kusikia ambayo wanatarajia kuitoa kwa wakazi wa Dar es salaam zaidi 2000 kwa muda wa siku nne katika Hoteli ya Serena.
Baadhi ya wakazi na watoto kutoka sehemu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam wakiwa katika foleni ya kupatiwa matibabu ya huduma ya vifaa vya kuwasaidia kusikia kutoka Mfuko wa Starkey Hearing leo jijini Dar es Salaam. Mfuko huo umeweka kambi katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo wanatarajia kutoa huduma hiyo bure kwa watu zaidi ya 2000 kwa kipindi cha nne.
Na Lorietha Laurence-MAELEZO, Dar es Salaam
ZAIDI ya wakazi 2000 wa Jiji la Dar es Salaam wenye matatizo ya kusikia wanatarajiwa kupata huduma ya vifaa vitakavyowasaidia kusikia vizuri. Huduma hiyo inatarajiwa kutolewa na Mfuko wa Starkey Hearing kwa muda wa siku nne katika Hoteli ya Serena iliyopo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mwanzilishi wa Mfuko huo, William Austin alisema mfuko wake unatambua kuwa sikio ni kiungo muhimu kwa binadamu ndio maana mfuko wake umeamua kuwasaidia watu mbalimbali wenye ulemavu wa kusikia duniani waweze kusikia na wasionekane wametengwa.
“Mimi nimeoma muda wangu mwingi katika kuwasaidia watu wasio na uwezo katika kuwapatia vifaa ambavyo kiasi kikubwa vitawaunganisha na watu wengine na hivyo kushiriki katika mijadala ya kuwaletea maendeleo yao na jamii yao,” alisema Austin.
Alisema kuwa umati uliojitokeza katika zoezi lao unaonesha kuwa wananchi wengi wanasumbuliwa na matatizo ya masikio na hivyo wanahitaji huduma ya vifaa ili waweze kuwasiliana na wenzao wasio na matatizo.
Alisema mpango huo umeanzia jijini Dar es Salaam ambapo utawawezesha kuhudumia watu 600 kila siku wenye matatizo kama hayo kwa muda wa siku nne. Jumla ya wagonjwa 2000 wenye matatizo ya kusikia wanatarajia kupata huduma hiyo jijini Dar es Salaam.