Watu 100 Wauwawa Sudan Kusini Baada ya Kushambuliwa

Jeshi la Sudan Kusini


WAKUU wa Sudan Kusini wanasema watu zaidi ya 100 wameuwawa kwenye wizi wa mifugo. Taarifa zinasema watu wa kabila la Lou Nuer walishambuliwa Ijumaa katika Jimbo la Mashariki la Jonglei, huku taarifa zaidi zikidai shambilizi hilo lilifanywa na watu wa kabila la Murle.

Umoja wa Mataifa (UN) unasema shambulio hilo ndio kubwa kabisa tangu mwaka wa 2011 ambapo watu wa kabila hilo zaidi ya 100 waliuliwa na vijana wa Lou Nuer.

Wadadisi wanasema tangu Sudan Kusini kupata uhuru mwaka huo, nchi hiyo imekuwa na shida ya kudhibiti maeneo hayo ya mbali ambayo yana silaha nyingi baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miongo miwili.
-BBC