Watoto Wakifanya ‘Maajabu’ Ndani ya Maonesho ya Wiki ya Ndenda kwa Usalama

Mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya Msingi
Malangali, iliyopo mkoani Iringa, Steven Mligo akitoa elimu kwa watoto wenzake
juu ya Usalama barabarani na namna mbalimbali za matumizi sahihi ya barabara
ikiwa ni pamoja na kutambua alama mbalimbali za barabarani. Mligo alikuwa
akitoa elimu hiyo katika banda la Polisi Trafiki lililopo katika maonesho ya
Wiki ya Nenda kwa Usalma Kitaifa inayofanyika Mkoani Iringa katika uwanja wa
Samora.


Mtaalam wa Elimu kutoka Mfuko wa Elimu Manispaa ya Iringa, Germana Kapinga (kulia) akimsikiliza mkazi wa mjini Iringa aliyetembelea banda lao lililopo katika maonesho ya Wiki ya nenda kwa Usalama viwanja vya Samora mjini Iringa.
 Wakazi wa mjini Iringa wakiwa katika banda la ASAS wakijipatia bidhaa mbalimbali zitokanazo na maziwa.

 Kwa lugha fasaha unaweza kumuita Fahari! Huyu dume la Ngombe ambalo linakadiriwa kuwa na uzito wa zaidi ya kilo 1000, akiwa katika maonesho ndani ya banda la ASAS DAIRY FARM katika uwanja wa Samora mjini Iringa yanapoendelea maonesho ya Wiki ya Nenda kwa Usalma kitaifa.
 Wakazi mbalimbali mjini Iringa, wakiangalia Ng’ombe katika banda la ASAS DAIRY FARM
katika uwanja wa Samora mjini Iringa yanapoendelea maonesho ya Wiki ya Nenda kwa Usalma Kitaifa.