Watoto wa Mitaani Waliotwaa Ubingwa wa Dunia, Waomba Kuendelezwa…!

Kipa bora wa Timu ya Watoto wa Mitaani (TSC) na Kapteni Msaidizi Emmanule Amos akipeana mkono na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi mjini Dodoma mara baada ya timu hiyo na viongozi wao kutembelea Bunge Maalum la Katiba.

Kipa bora wa Timu ya Watoto wa Mitaani (TSC) na Kapteni Msaidizi Emmanule Amos akipeana mkono na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi mjini Dodoma mara baada ya timu hiyo na viongozi wao kutembelea Bunge Maalum la Katiba.


Timu ya Watoto wa Mitaani (TSC) ikiwa katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma mara baada ya  timu hiyo na viongozi wao kutembelea Bunge Maalum la Katiba.

Timu ya Watoto wa Mitaani (TSC) ikiwa katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma mara baada ya  timu hiyo na viongozi wao kutembelea Bunge Maalum la Katiba.

Na Magreth Kinabo – Dodoma
 
MFUNGAJI bora wa Timu ya Watoto wa Mitaani kutoka Mwanza Tanzania, iliyotwaa ubingwa wa dunia(TSC) katika mashindano ya Kombe la Dunia la Watoto hao yaliyofanyika Brazil, Frank William ameishauri Serikali na wadau wengine kuwasaidia watoto hao na wengine wa mitaani kuweza kukuza vipaji vyao.

William ametoa kauli hiyo mjini Dodoma wakati timu yao ilipotembelea Bunge Maalum la Katiba Mjini Dodoma, wakiwa na viongozi wao, ambapo walipata nafasi ya kuzungumza na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara pamoja na Naibu wake Juma Nkamia.

Mchezaji huyo alisema siri ya ushindi wetu ni ushirikiano na kujituma, tukilikwenda kuwakilisha watoto wengine wa mitaani. Hivyo aliomba jamii kuwasaidia watoto wengi wa mitaani ambao hawana uwezo wa kupata elimu lakini wana vipaji mbalimbali ili waweze kuvikuza.

Kwa upande wake kipa bora wa timu hiyo, Emmanue  Amos, alishauri Serikal iweze kuwasaidia ili waweze kushiriki katika mashindano ya mwaka 2018 ya kombe hilo. Mchezaji mwingine wa timu hiyo, Denis David aishauri jamii isiwadharau kwa kuwa ni watoto wa mitaani kwani wanavipaji wakipata watu wa kuwasaidia, hivyo aliitaka iwekeze katika soka la vijana kwa sababu baada ya miaka 20 ijayo mchezaji bora anapatikana kwa njia hiyo.

Aliwaomba wajumbe wa  Bunge  hilo, kuwasaidia ili waweze kuvikuza vipaji vyao. Naye Kocha wa timu hiyo, Suileiman Jabir alisema wadau mbalimbali kuwasaidia na kuwaendeleza watoto hao I, ambao ni wengi ambao wanaweza kuwa na vipaji vya sanaa na utamaduni.

Akizungumzia kuhusu mafanikio ya ushindi huo, ni kuwa na mpango wa kutafuta vijana wenye vipaji ambapo wanaviendeleza na kuvikuza kwa kufanya maandalizi ya kiutalaamu na kiufundi. Jabir aliongeza kuwa waliwandaa kisaikolojia ili waweze kushinda katika mashindano hayo ya kimataifa.

Aidha aliwataka wajumbe wa Bunge hilo, kuhakikisha wanalipa kipaumbele suala la kuweka sheria itakayo wadhibiti wakina baba wanaotekeleza watoto, huku akiiasa jamii kuwasaidia watoto pale wazazi au walezi wanapofariki dunia. Naye Rais wa timu hiyo, Altaf Hirani ameiomba Serikali kuweza kuwasaidia kupata kiwanja cha michezo  kwa ajili ya watoto jijini Mwanza au kwenye  maeneo mengine ya nchi.