Watoto 40 wapata Kipaimara St. Joseph Dar es Salaam

Baadhi ya watoto waliopewa daraja la Kipaimara jana katika Kanisa la St. Joseph wakiwa katika ibada ya kupewa daraja hilo jana jijini Dar es Salaam

Baadhi ya watoto waliopewa daraja la Kipaimara jana katika Kanisa la St. Joseph wakiwa katika ibada ya kupewa daraja hilo jana jijini Dar es Salaam

Baadhi ya waumini akiwemo Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa akiwa katika ibada hiyo jana

Na Mwandishi Wetu

ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam ametoa Daraja la Kipaimara kwa watoto 40 kutoka Parokia ya St. Joseph ambao wamefanikiwa kufuzu katika mtihani wa mafunzo wa daraja hilo.

Akiongoza ibada maalumu ya kuwavisha daraja hilo jana jijini Dar es Salaam, Mhashamu Askofu Eusebius Nzigirwa aliwataka vijana hao na waumini wengine kuwa imara na kujitoa pale inapobidi katika kumtumikia Mungu.

Alisema wananchi wengi wamekuwa wakitoa vipaumbele zaidi katika mambo ya kiulimwengu na kumsahau Mungu. “Wapo watu ambao wanafanya kazi kiasi kwamba hata inapofikia kwenda Kanisani wanajifanya hawana nafasi, akiambiwa akasali kwenye Jumuiya anasema hana nafasi…lazima utenge muda wa kumushukuru Muumba,” alisema Baba Askofu.

Aidha aliwataka waumini kuishi kwa kuvumiliana na kusamehe pale wanapoitilafiana kwani kwani ni jambo la kawaida kwa watu kupishana kimawazo na mtizamo katika maisha.