Na Magreth Kinabo –Maelezo
Serikali imewataka watendaji wote afya wa halmashauri ,mikoa wilaya kusimamia suala la usafi wa mazingira ilikuizesha jamii kuepukana na matatizo ya milipuko ya magonjwa likiwemo suala la ugonjwa wa kipindupindu.
Aidha Serikali pia imewataka watendaji hao, kuanzisha siku maalum ya usafi katika maeneo wanayotoka.
Kauli hiyo imetolewa jana jioni na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Donan Mmbando wakati akifunga mkutano mkuu wa mwaka wa sekta ya afya ambao uliambatana na maadhimisho ya miaka 40 ya Mpango wa Taifa wa Chanjo uliofanyika kwenye hoteli ya kuanzia Septemba 8 hadi 11, mwaka huu Ubungo Plaza jijini Dares Salaam.
“Ni lazima tuwe na utaratibu huu mpya kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Wizara ya Maji, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) vyombo vya habari ili kuweza kutatua tatizo hilo,” alisema Dkt. Mmbando.
Aliongeza kwamba watendaji hao watakiwa kutoendelea kuruhusu vyakula kusafirishwa katika maeneo ya wazi, madimbwi ya maji machafu, usimamizi wa huduma za afya ufanyike ipasavyo.
“ Tusimamie mpango wa utekelezaji wa elimu ya afya mashuleni, likiwemo suala la vyoo ambalo limepewa walimu maalum wa kusimamia ,hivyo zamani tulikuwa tunakaguliwa kuhusiana na usafi wa mwili mashule mafano kuoga nna kuchana nyewele pia kuweka yanayotunguzuka kuwa safi mazingira. Turudi katika misingi hiyo tuaondokana na matatizo ya afya,” alisisitiza.
Dkt. Mmbando alisema kanuni na miongozi ipi ya kutosha hivyo, watendaji hao wanapaswa kuongeza kasi ya utendaji kazi na kushirikiana kwa pamoja katika kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza na kuambukiza ili kuweza kuiwezesha sekta ya afya kupata mafanikio makubwea zaidi katika kufikia malengo ya milinea(MDG’s ).
Aliongeza kwamba Mlipuko wa magonjwa ya kipindupindu umetokea katika mikoa ya Dares Salaam, Morogoro na Pwani na unatokana na tatizo la kutozingatia , misingi ya usafi wa mazingira husasan kwenye vinywaji, vyakula na mazingira yasiyosafi.