WATEJA wa Vodacom M-Mpesa wenye akaunti katika benki ya CRDB sasa wanauwezo wa kuweka na kutoa fedha kutoka katika akaunti zao kupitia simu ya mkononi ya Vodacom iliyosajiliwa na huduma ya M-Mpesa.
Kuzinduliwa kwa huduma hiyo sasa kunawapa urahisi zaidi wateja wa Vodacom M-Mpesa kuweka na kuchukua fedha zao kutoka akaunti ya benki kwa urahisi na unafuu zaidi mahali popote nchini na kwa wakati wowote pasi na kulazimika kufika katika tawi la benki ya CRDB..
Huduma hii ya ushirikiano kati ya Benki ya CRDB na kampuni ya Vodacom kupitia huduma yake ya M-Mpesa ni ya kwanza nchini na inalenga kuwaondolea usumbufu wateja wa M-Mpesa wa kupanga foleni ama kutembea umbali mrefu kufuata tawi la Benki.
“Tunapoitambulisha huduma hii mpya inaamaanisha kwamba tumeongeza thamani nyengine katika simu ya mkononi na huduma ya Vodacom M-Mpesa. Mteja wa M-Mpesa kuweza kutoa na kuchukua fedha kutoka akaunti zao za CRDB kupitia simu zao za mkononi ni hatua nyengine muhimu ya kujivunia kuwa mteja wa Vodacom”Alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Bw. Rene Meza.
Huduma ya Vodacom M-Mpesa ya kwanza sokoni kutoka Vodacom mtandando unaoongoza nchini ni kielelezo makini cha ubunifu na namna ambavyo Vodacom imedhamiria kubadili maisha ya watu kupitia teknolojia ya simu za mkononi.
Ikiwa na mawakala zaidi 20,000 nchi nzima M-Mpesa inabakia kuwa huduma salama zaidi, ya haraka, uhakika na yenye kuaminika kwa ajli ya kuweka na kutuma fedha, kufanya malipo ya huduma na manunuzi mbalimbali, kulipia kodi, kuchangia pensheni pamoja na kupokea fedha kutoka nchi zaidi ya sabini na tano ulimwenguni.
“Hakuna mteja wa Vodacom M-Pesa atakaesimama kwenye foleni au kulazimika kutembea umbali mrefu kufuata tawi la benki yake ya CRDB, sasa wataweka na kutoa fedha wakati wowte na mahali popote bila kuathiri shughuli nyengine za kijamii na kimaendeleo ni wazi maisha yamekuwa rahisi zaidi.”Aliongeza Bw. Rene
Tangu ilipoanzishwa mwaka 2007, huduma ya Vodacom M-Mpesa imeendelea kujipatia umaarufu mkubwa kutokana na kuwa huduma yenye usalam zaidi, yenye mtandao mpana wa mawakala mijini na vijijini na hivyo kuchangia maendeleo ya jamii na biashara nchini kwa kuinua vipato vya wananachi kupitia ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja.
Kuweka fedha katika akaunti ya CRDB kutoka akaunti ya M-PESA,hatua ni kama ifuatavyo
I. Piga *150#
II. Chagua kulipia bili
III. Ingiza namabri ya biashara ambayo ni 900500
IV. Ingiza nambari ya kumbukumbu ambayo ni namabri ya akaunti ya benki.
V. Weka kiasi cha fedha mteja anachotaka kutoa katika akaunti ya M-PESA kwenda akaunti ya benki
VI. Ingiza nambari ya siri.
VII. Bonyeza 1 kuthibitisha au 2 kubatilisha muamala.
Baada ya hatua hizi mteja atapokea mara moja ujumbe mfupi wa maneno – SMS kutoka M-PESA kuthibitisha muamala na baada ya dakika 8 atapokea ujumbe kutoka benki ya CRDB.
Kuhamisha fedha kutoka akaunti ya Benki ya CRDB kwenda M-PESA hatua ni kama ifuatavyo
I. Piga *150*03#
II. Ingzia nambari ya siri
III. Chagua nambari 3 (Hamisha fedha)
IV. Chagua nambari 3 (M-PESA)
V. Chagua nambari ya akaunti yako ya Benki
VI. Thibitisha nambari yako ya simu
VII. Ingiza kiasi cha fedha unachotaka kuhamisha
VIII. Thibitisha au batilisha. Na baada ya hapo utapokea ujumbe mfupi wa maneno – SMS kutoka M-PESA na pia Benki ya CRDB unaothibitisha zoezi hili.
Ili kuwa na uwezo wa kuhamisha fedha kutoka Benki kwenda M-PESA ni LAZIMA kwanza mteja wa M-PESA ajisajili CRDB.
Usajili huo hufanyika MARA MOJA TU na kwamba unaweza kufanyika kupitia simu ya mkononi kwa kupiga *150*03# na maelezo ya namna ya kujisajili yatatotekea ambayo mteja atapaswa kuyafuata.