Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel imeendelea kuboresha huduma ya Airtel Money kwa kurahisisha upatikanaji wa muongozo (menu) kwa kupiga *150*60# Bure pamoja na kuzindua promosheni kabambe itakayowawezesha wateja wa Airtel nchi nzima kutuma pesa bure.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa huduma hiyo, Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando alisema Airtel inaendelea kutoa uhuru kwa wateja kupata huduma kirahisi zaidi nchini kote, na kuanzia sasa mteja akipiga *150*60# anapelekwa moja kwa moja kwenye orodha yake ya huduma na kuweza kuchagua anachohitaji kufanya ikiwa ni pamoja na kuongeza salio, kufanya malipo, kutoa pesa na mengine mengi.
“tumefanya hivi hii ili kumwezesha mteja mwenye simu yeyote kupata huduma za kibenki na kuondoa changamoto zozote zitakazojitokeza, sasa mteja anauhuru wa kuchagua kutumia njia ya awali ambayo ni kwenda mojakwa moja kwenye muongozo wa simu yake na kupata horodha (Menu) ya Airtel au kupiga namba *150*60# na kuunganishwa moja kwa moja,” alisema.
vilevile alisema kampuni hiyo imezindua ofa kabambe kwa wateja nchini zima ambapo kutuma au kupokea pesa chini ya kiwango cha 100.000 ni BURE na mteja atakaponunua LUKU kupitia Airtel money ni BURE (hakuna viwango vya miamala vitakavyotozwa). Tunawajulisha wateja wetu wote na wakala wetu waliosambaa nchi zima kutumia huduma hii iliyorahisi ni rahisi aliongeza,” Mmbando.
“Airtel ni mtandao ulioenea nchini na unatoa huduma za kifedha za Airtel money yenye mawakala zaidi ya 10,000 waliosambaa maeneo mbalimbali mjini na vijijini kwa dhamira ya kupunguza changamoto ya upatikanaji wa huduma za kifedha na kusaidia wateja wetu kuokoa muda kwenda mbali kupata huduma za kibenki.”
“Kupitia Airtel money mteja anaweza kupata huduma mbalimbali ikiwemo: kupokea pesa, kulipa bill kama DSTV, LUKU na DAWASCO, USA visa, kununua salio na huduma nyingine nyingi.”