TAKRIBANI watu watatu wameuawa katika shambulio mashariki mwa Kenya na zaidi ya watu 27 wamejeruhiwa kwenye shambulio la guruneti katika mji wa Garissa, karibu na mpaka wa Somalia.
Awali, mwanajeshi wa Kenya aliuawa katika mlipuko wa bomu katika mji wa mpakani wa Mandera.
Wanajeshi wa Kenya wako nchini Somalia tangu mwezi Oktoba kukabiliana na waasi wa kundi la al-Shabab ambao wanasema walishambulia maafisa wao wa usalama na watalii nchini Kenya.
Katika moja ya shambulio kwenye hoteli mjini Garissa, huku shambulio jingine katika barabara za mji huo likasababisha kifo cha mtu wa tatu, vyanzo vya polisi vilisema. Watu kumi na mbili walijeruhiwa vibaya.
” Wawili walifariki dunia katika hoteli ya Holiday Inn inafahamika na wakaazi kama Kwa Chege. Mwingine alifariki dunia katika shambulio kwenye barabara inayofahamika kama ya Ngamia,” afisa wa polisi alisema.
Alipoulizwa nini kilisababisha mlipuko huo, alisema: ” Haya yalikuwa maguruneti”, akiongeza kuwa wengine ya wale waliojeruhiwa ni kutokana na maguruneti hayo.
Mkaazi mmoja wa eneo hilo Hussein Abdi ameliambia shirika la habari la AFP kulikuwa na hali ya taharuki katikati mwa mji huo sehemu ambay mlipuko ulitokea.
Mji wa Garissa ni mji mkuu wa mkoa wa Kaskazini mashariki, na uko kilomita 100 (maili 60) kutoka mpaka wa Somalia.
-BBC