Watatu Wakwea Pipa na Serengeti Premium Lager, Ni Promosheni ya Winda Safari ya Brazil

Washindi wa safari ya Brazil wakipunga mkono kwa bashasha mda mfupi kabla ya kukwea pipa kuelekea nchini Brazil. Washindi hawa watakula bata siku tano nchini Brazil. Kulia ni Deusdedit Kahwa kutoka  Dar es salaam, Juliana Masawe kutoka Moshi(wa pili kulia)kushoto ni Meneja Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti Bw. Allan Chono na wa pili kulia ni Menrad Shayo kutoka Arusha.

Washindi wa safari ya Brazil kupitia promosheni ya Winda Safari ya Brazil na Serengeti katika picha ya pamoja huku wakisubiri kuelekea nchini brazil kula  bata. Kulia ni Deusdedit Kahwa kutoka  Daer es salaam, Juliana Masawe kutoka Moshi (wa pili kulia) kushoto ni Meneja Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti Bw. Allan Chono na wa pili kulia ni Menrad Shayo kutoka Arusha.

WASHINDI watatu wa promosheni ya ‘Winda Safari ya Brazil na Serengeti’ iliyokuwa ikiendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti hatimaye waliondoka wiki iliyopita kuiona Brazil ili kutimiza ndoto zao kwa kushuhudia live vivutio mbalimbali vinavyopatikana nchini humo. Promosheni hii ilianzishwa na kampuni ya bia ya Serengeti kwa lengo la kuwapa furaha wateja wao na kurudisha faida kwa wateja ambao ndio nguzo kubwa ya mafanikio ya kampuni hiyo.

Washindi wa tiketi hizo Bi Juliana Joseph Masawe kutoka Kilimanjaro, Deusdedit Kahwa kutoka Dar es Salaam pamoja na Menrad Faustin Shayo kutoka Arusha walijishindia tiketi hizo baada ya kutumia bia ya Serengeti Premium Lager na kufungua chini ya kizibo ili kushinda.

Washindi wa safari ya Brazil wakiondoka katika uwanja wa ndege wa mwalimu Julius Nyerere huku wakiongozwa na Meneja Masoko wa  kampuni ya bia ya Serengeti  Bw. Allan Chonjo.

Washindi wa safari ya Brazil wakiondoka katika uwanja wa ndege wa mwalimu Julius Nyerere huku wakiongozwa na Meneja Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti Bw. Allan Chonjo.

Meneja masoko kampuni ya bia ya Serengeti Bw. Allan Chonjo ambaye ameambatana na washindi hao nchini Brazil aliwashukuru watumiaji wa kinywaji cha Serengeti kwa kuwa wateja wao wa kuaminika na aliwasisitiza kuendelea kutumia kinywaji hicho ili kuendelea kujipatia zawadi mbalimbali katika promosheni zinazotolewa na kampuni hiyo.
“Tutakuwa nchini Brazil hadi tarehe 17 Juni tukishuhudia vivutio vinavyopatikana nchini haswa msitu mkubwa wa Amazon na kwa muda huo wote kampuni ya bia ya Serengeti itahusika na kugharamia gharama zote za washindi kipindi watakachokuwa nchini humo kuanzia makazi, malazi afya na usalama hadi watakaporudi.”

Bi Juliana Joseph Masawe amejivunia kutumia bia ya Serengeti Premium Lager na ameishukuru kampuni ya bia ya Serengeti kwa kumpa fursa kubwa ya kusafiri kwenda Brazil “Mimi napenda sana kutembelea sehemu mbalimbali na kushuhudia vivutio sijawahi kupata fursa kama hii ya kutoka nje ya nchi yangu kwenda kujionea vivutio, ila sasa ninaamini nitafurahia vitu vingi kwani pamoja na kuwa ni mara ya kwanza kwenda nchi za nje, nitapata fursa ya kutembelea vivutio mbalimbali vya nchini Brazil na ninaamini nitaiwakilisha nchi yangu vizuri kwa kutangaza vivutio vyetu pia. Nawashukuru sana kampuni ya bia ya Serengeti kwa kutupa ofa hii kubwa”. Alieleza Bi Masawe.

Ofa hii ya tiketi za kwenda Brazil kushuhudia vivutio vinavyopatikana nchini Brazil kupitia promosheni ya “Winda Safari ya Brazil na Serengeti” inawapa fursa wateja wa bia hiyo ya Serengeti kuburudika na kujivunia kutumia bia hiyo kwani kampuni ya bia ya Serengeti inawathamini wateja wake na hivyo zawadi ya tiketi hizo ni wajibu wa kurudisha faida kwa wateja na kuwataka wateja wa bia hiyo kuendelea kutumia bia hii ya Serengeti Premium Lager kwani ni bonge la kiburudisho. Kunywa pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya yako. Tafadhali kunywa kistaarabu.