Watanzania wasikate tamaa kupoteza mechi za mwazo-SBL

Mkurugenzi wa Masoko wa SBL akizungumza na wanahabari leo uwanja wa Taifa.

Na Mwandishi Wetu

WADHAMINI wakuu wa Mashindano ya Kombe la Tusker Chalenji Kampuni ya Bia ya Serengeti Breweries Ltd (SBL) wamewataka Watanzania na wadau wa Soka nchini kutokata tamaa a timu za Tanzania kupoteza mechi zao za kwanza.

Kauli hiyo imetolewa leo katika Uwanja wa Taifa na Mkurugenzi wa Masoko wa SBL, Phraim Mafuru alipokuwa akizungumza na wana habari mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa timu ya Kilimanjaro Stars ya Tanzania na Rwanda ambapo Rwanda imezinda 1-0.

Alisema kupoteza michezo hiyo ya awali kusiwakatishe tamaa kwani bado wananafasi ya kufanya vizuri katika mechi zinazofuata. Alisema kinachotakiwa ni Watanzania kujitokeza na kuziunga mkono timu zao kwa kuzishangilia zaidi ili ziweze kufanya vizuri katika michezo inayofuata.

“Sisi tunaamini Tanzania bado inanafasi ya kufanya vizuri hivyo kinachotakiwa ni wapenzi na mashabiki tujitokeze na kuwashangilia kwa nguvu. Naye Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Richard Well amesema nia ya wao kudhamini mashindano hayo ni kuhakikisha timu hizo zinapata uzoefu wa kutosha hivyo kufanya vizuri katika michezo yao ya mbele.

SBL imedhamini Mashindano ya Tusker Chalenji yanayoendelea sasa kwa kiasi cha fedha zaidi ya milioni 900.