Watanzania Wanaoishi Ujerumani Kukutana na Wafadhili 150

Nembo ya Jumuiya ya Watanzania Waishio Ujerumani

UMOJA wa Watanzania nchini Ujerumani (UTU) Unapenda kuwakaribisha Watanzania wote wanaoishi ujerumani, Katika Hafla ya WORLD MISSION SUNDAY. itakayofanyika Katika ukumbi Uliopo Hauptstr. 30, D-63814 Mainaschaff Jirani sana na Mji wa Aschaffenburg Siku ya Jumapili Tarehe 28.10.2012, Kuanzia saa 04:00 za Asubuhi.
Ambapo Wasamaria wema na Wafadhili wapatao zaidi ya 150 kutoka sehemu mbali mbali za ujerumani watakutana na umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU) Juu ya kuitakia mema Tanzania na kuanzisha Harambee ya kuchangia maendeleo ya miradi mbali mbali itakayosimamiwa na Umoja wa watanzania Ujerumani (UTU).
Katika Hafla hiyo Kuanzia saa 9 mchana watayarishaji wa Hafla hiyo ”World Mission Sunday” itatoa nafasi kwa Umoja wa Watanzania Ujermani (UTU) Kuitambulisha Tanzania Kwa wahisani hao , na kuelezea ni mradi gani unahitaji ufadhili kupitia Umoja huu. Mmoja wa wageni rasmi walio alikuwa ni Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Ahmada Ngemera, Dk. Lippert na mkewe Kutoka Scheinfurt’ Dk. Lippert ni mtaalamu ambaye aliwahi kufanya kazi Tanzania.
Hafla hii inategemewa kuisha saa 12:00 za jioni, baada ya hapo watanzania watapata muda wao wa kufanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania Nchini Ujerumani, Ahmada Ngemera.

Umoja wa Watanzania Ujerumani UTU Umeramba Bingo kwa kupewa nafasi hii ya pekee Na WORLD MISSION SUNDAY Kuiwakilisha Jamii ya watanzania na kuwashawishi Wafadhili na wahisani nchini ujerumani ili waweze kuchangia Miradi mbalimbali ya Huduma za jamii nchni Tanzania ikiwemo sekta ya Elimu na Afya.

Tunawaomba Watanzania Wote na marafiki wa Tanzania wanaoishi Ujerumani na jirani mwa ujerumani, kuhudhuria kwa wingi katika Hafla hii muhimu kwa jamii ya watanzani kama wasemavyo wahenga ”CHEREKO CHEREKO NA MWENYE MWANA” Kwa maelezo zaidi wasiliana na kamati.utu@googlemail.com au unaweza kuwasiliana na Mwenyekiti Wa UTU moja kwa moja kupitia simu ya mkononi. 0173-4298997
Karibuni sana ! Umoja Ni Nguvu