Watanzania waishio Ujerumani kufanya hafla ya kumuaga Mhe,Balozi Bw.Ahmada Ngemera

Umoja wa Tanzania Ujerumani (UTU) unaheshima kubwa kutarifu na kuwaomba watanzania wote
wanaoishi ujerumani na jirani ya Ujerumani kuwa umoja wetu tunatarajia kufanya afla ya kumuaga
Mheshimiwa balozi Bw. Ahmada Ngemera ambaye anamaliza mda wake wa kufanya kazi,
Afla hiyo itafanyika mjini Berlin siku ya Jumamosi tarehe 8.12.2012 .
Mhe.Balozi bwana Ahmada Ngemera amekua balozi wa Tanzania nchini Ujerumani na watanzania
wanaoishi ujerumani watamkumbuka daima Mheshimiwa Balozi Bw.Ahmada Ngemera kwa kuwa
karibu sana na jamii ya watanzania,pia atakumbukwa kwa jitihada zake au kile ambacho watanzania
wa ujerumani wanachokiita kuasisi Umoja na mshikamano wa watanzania nchi ujerumani,ambapo
Mhe.Balozi Bw.Ngemera na msaidizi wake Mhe.Bw.Ali Siwa wahamua kuhamasisha watanzania
waishio Ujerumani kuungana katika kila hali kuanzisha umoja wa mshikamano wa watanzania,kitu
ambacho mabalozi wengi walishindwa kufanikiwa kufanya labda kwa sababu ya ukubwa wa nchi ya
ujerumani wa watanzania wanaishi katika miji mbali mbali,lakini kazi hiyo ya kuwaungunganisha
watanzania, Balozi Bw.Ahmada Ngemera na Msaidizi wake Bw.Ali Siwa walifanikiwa kuwafikia
watanzania wote waishio Ujerumani na kuwashauri waanzishe umoja wa mshikimano,na matunda
ya juhudi zao ndipo kukazaliwa Umoja wa waTanzania Ujerumani.(UTU) Umoja ambao ni chombo
cha watanzania wote ! chombo ambacho watanzania waishio ujerumani wanajivunia !
UMOJA NA MSHIKAMANO NDIO MSINGI WETU IMARA!
OMBI:
TUNAWAOMBA WATANZANIA WOTE ! NA MARAFIKI WOTE WA TANZANIA
AMBAO WANATAKA KUSHIRIKI KATIKA AFLA HII,
TUNAOMBA MTOE MCHANGO WA EURO 20.00 NA KWA WANAFUNZI EURO 10.00 TU