Watanzania Wahimizwa Kutumia Mbinu Mpya za Kutambua Bidhaa Feki

Pambika na Samsung

Pambika na Samsung

BIDHAA feki zimekuwa moja kati ya tatizo kubwa linaloikumba soko la Tanzania tatizo linaloletwa na kile kinachoitwa soko huria, wateja wa bidhaa mbalimbali wamekuwa wakipata hasara kutokana na bidhaa kushindwa kufanya kazi kutokana na uwezo mdogo au bidhaa hiyo kuharibika mapema mara baada ya kununuliwa dukani na kumuacha manunuzi akilalamika bila ya msada wowote ama kwa kutojua nini cha kufanya au kwa kutakuwa na matumaini ya kupata msaada kutoka kwa mamlaka husika.

Sekta mbalimbali zimeshaanza juhudi za kukabiliana na tatizo la bidhaa feki kwa kuvumbua mbinu na mikakati itakayokabiliana na tatizo lilopo sokoni hivi sasa. Makampuni makubwa hasa yale yanayotengeneza simu za mkononi yameshaanza kutoa huduma Maalum za kubaini simu halisi mara mtu anaponunua katika maduka mbalimbali. Kuongezwa kwa muda wa huduma ya mkataba wa bidhaa kwa lugha ya kigeni “Warranty” mara mtu anaponunua ni moja kati ya mbinu hizo pamoja na kusajili simu mpya mara inaponunuliwa, huduma hizi zote zinalenga kupambana na simu feki.

Kwa kutumia mbinu za kipekee katika kuhamasisha watu kutonunua bidhaa feki au iliyoibiwa na kumpa mteja nafasi ya kuangalia uhalisia wa bidhaa husika aliyonunua, kampuni kama Samsung imetambulisha huduma yake ya “E-Warranty” ya miezi 24 kutoka miezi 12. Mteja aliyejisajili na huduma ya E-warranty mara baada ya kuinunua bidhaa ya Samsung atapata huduma za ukarabati wa bidhaa yake ndani kwa miaka bure mara tatizo lolote linapotokea, iwe tatizo hilo linalotokana na bidhaa yenyewe au mtuamiaji wake kuharibu bidhaa hiyo.     

Huduma hii ya kusajili bidhaa yako kwenye e-warranty imerahisishwa zaidi, mara mteja anaponunua bidhaa halisi anaweza kujisajili kwa kutumia simu yake kupitia mitandao yote hapa nchini. Katika bidhaa za simu mteja wa Samsung anatakiwa kusajili simu yake katika huduma ya e-warranty kwa kutuma ujumbe wenye namba maalum zenye uwezo wa kujua mahala simu hiyo iliponunuliwa (IMEI) kwenda 15685, namba hizi Maalum ambazo ni 15 zinapatikana nyuma ya kasha la simu au nyuma ya simu yenyewe. 

Katika kuhamasisha Watanzania wananunua bidhaa halisi na kuzisajili, Samsung Tanzania imetangaza kuanza kwa promosheni yake kubwa katika msimu huu wa mwisho wa mwaka kwa kuwazawadia wateja watakaonunu bidhaa halisi na kuzisajili, wateja hao wataingia kwenye droo ya kila wiki  na kuwa na nafasi ya kujishindia bidhaa mbalimbali za Samsung.

“Hofu yetu kubwa imekuwa katika madhara wanayowapata Watanzania kwa kutumia bidhaa feki, bidhaa feki zipo sokoni na ili kuonyesha tunawajali wateja ni Lazima tupambane na tatizo hili, tumetambulisha huduma ya e-warranty ambayo inampa nafasi mteja kwa kuangalia uhakika wa bidhaa aliyonunua kwamba si feki” alisema Bw. Kishor Kumar, Meneja wa Samsung Tanzania Kitengo cha Simu na Teknolojia ya Habari.
Pambika na Samsung ni promosheni ya nchi nzima ambayo imeanza Novemba 7 mpaka Decemba 23, 2013.

Promosheni hii inalengo la kuwazawadia wateja wapya wa Samsung wakati huo huo ikihamasisha wateja kuinunua bidhaa halisi na kuzisajili katika huduma ya e-warranty ili kufaidi huduma zake bure ndani ya miaka miwili.