Watanzania Ujerumani kushangweka na miaka 50 ya Uhuru!

Bango la miaka 50 Uhuru

Chereko chereko zitaanzia München hadi Berlin

BENDI ya Ngoma Africa a.k.a FFU Desemba 10, 2011 inatarajia kutoa burudani ya kukata na soka kwa Watanzania wa Umoja wa Tanzania Ujerumani (UTU) kuzinduliwa rasmi!

Watanzania waishio Ujerumani wameanza shamra shamra za kusherekea miaka 50 ya uhuru wa Tanzania bara, kwa kasi kubwa inayotingisha kila kona, sherehe hizo zinaanzia mjini München siku ya Desemba 3, 2011 ambapo kutakuwa na maonyesho mbali mbali ya bidhaa za Tanzania, mavazi, na mdahalo rasmi na usiku kutakuwa na muziki wa Ngoma Africa Band katika Mtaa wa Siebold Str, 11 ndipo penye ukumbi.

Kuanzia Desemba 9 hadi 10, 2011 mjini Berlin ambako ndipo hupo Ubalozi wa Tanzania na ndio Mji Mkuu wa Ujerumani, kutakuwa hapatoshi kwani sherehe hizo zitaambatana na ufunguzi wa Umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU) siku ya Desemba 10, 2011, umoja huo unawaunganisha Watanzania wote waishio ujerumani, ulitiliwa nguvu na Balozi Ngemera, umeshasajiliwa na viongozi wake ni Mfundo Peter Mfundo (Mwenyekiti).

Tullalumba Mloge (katibu), utaratibu unaonyesha kuwa sherehe hizo mjini Berlin zitaanza saa 9 mchana hadi usiku usio kwisha ambapo Ngoma Africa Band aka FFU, watatumbuiza na muziki wao, mahala patakapo fanyika sherehe Apostelkirche 1, 10738 Berlin. Umoja ni Nguvu Watanzania Jitokezeni! Kushrekea miaka 50! sikiliza muziki at www.ngoma-africa.com