Berlin, Ujerumani
UMOJA wa Watanzania Ujerumani (UTU) unatarajia kufanya Mkutano Mkuu wa uchaguzi siku ya kilele cha Sherehe za Muunganno wa Tanganyika na Zanzibar mjini Berlin, Ujerumani. Mkutano huo utafanyika Aprili 26, 2014 kuanzia saa 7 mchana katika ukumbi wa Deutsche Bank, Unter den Linden 13-15, 10117 Berlin, Ujerumani.
Watanzania wote wanaoishi Ujerumani wanaombwa kuhudhuria kwa wingi katika mkutano huu muhimu wa chombo chao UTU ambao kinawaunganisha watanzania wote waishio ujerumani bila kujali itikadi zao za kidini, jinsia, wala kabila.
Umoja wa watanzania ujerumani unafuraha kubwa ya kuwafungilia milango wale wote ambao wanataka kujiunga na umoja huo. Pia milango ipo wazi kwa wadau na wale wote wanaohitaji ushauri juu ya kuwekeza au kuchangia maendeleo ya jamii nyumbani Tanzania. Pia pata kuwepo na vyakula vya Kitanzania
KUFIKA KWENU KATIKA MKUTANO HUU NDIO MAFANIKIO YA WATANZANIA WOTE
UMOJA NI NGUVU, UTENGANO NI UDHAIFU
UMOJA WA KITAIFA NDIO MSINGI IMARA KWA WATANZANIA
MUNGU IBARIKI TANZANIA