Watanzania Ughaibuni Watakiwa Kuwekeza Kwenye Afya Tanzania

Waziri wa Afya wa Tanzania, Seif Rashid (wa pili kulia) akiwa na baadhi ya Watanzania waishio nchini Ujerumani mara baada ya mkutano nao.

Waziri wa Afya wa Tanzania, Seif Rashid (wa pili kulia) akiwa na baadhi ya Watanzania waishio nchini Ujerumani mara baada ya mkutano nao.

Waziri wa Afya wa Tanzania, Seif Rashid, Waziri wa Afya Zanzibar, Rashid Seif Suleiman (aliye simama) wakizungumza na Watanzania waishio nchini Ujerumani (hawapo pichani).

Waziri wa Afya wa Tanzania, Seif Rashid, Waziri wa Afya Zanzibar, Rashid Seif Suleiman (aliye simama) wakizungumza na Watanzania waishio nchini Ujerumani (hawapo pichani).

Waziri wa Afya wa Tanzania, Seif Rashid (aliye simama) akizungumza na Watanzania waishio nchini Ujerumani (hawapo pichani).

Waziri wa Afya wa Tanzania, Seif Rashid (aliye simama) akizungumza na Watanzania waishio nchini Ujerumani (hawapo pichani).

WAZIRI wa Afya na Ustawi wa Jamii wa Tanzania, Seif Rashid na Waziri wa Afya wa Zanzibar, Rashid Seif Suleiman, Januari 25, 2015 walikutana na kuzungumza na na baadhi ya Watanzania waishio nchini Ujerumani.

Mkutano huo ulifanyika katika Hoteli ya Martim mjini Berlin, ambapo mawaziri hao kwa pamoja wakiwa na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Philip Malmo walitumia fursha kuzungumza masuala mbalimbali.

Katika mkutano huo kwa ujumla mawaziri hao walielezea jinsi wizara zao zinavyofanya kazi kuhakikisha huduma za afya zinawafikia walio wengi na pia kuhakikisha siku za usoni kila Mtanzania ananufahika kiufasaha na huduma hizo kwa kutumia mfumo wa bima ya afya bila kujali tofouti za uwezo wa vipato vyao.

Watanzania waishio Ujerumani wamefarijika kwa kitendo cha kufanyika kwa mazungumzo hayo, hivyo mawaziri wamewataka Watanzania waishio ughaibuni kuchangia kuwekeza katika sekta ya huduma ya afya hata ikiwa ni sekta binafsi kwani milango ya wizara zao ipo wazi kwa Watanzania wanaotaka ushauri, ushirikiano au kuwekeza katika sekta hizo.