Nyimbo za “Supu ya Mawe” na “Uhuru wa Habari” Kutinga Redioni
Wakati tunapoelekea katika shamra shamra za Siku Kuu ya Sabasaba,
Watanzania watafurahia sikuu hii kwa kupata burudani ya nguvu ya nyimbo
mpya zilizopo katika CD ‘Bongo Tambarare’ kutoka kwa bendi maarufu ya
muziki wa dansi.
Ngoma Africa Band a.k.a FFU yenye maskani nchini Ujerumani, CD hiyonyimbo tatu “Bongo Tambarare”, “Supu ya Mawe” na “Uhuru wa Habari”. Inasemekana imeshaanza kupiga hodi katika milango ya vituo mbali mbali vya redio
duniani na hapa nyumbani itasikika wakati wowote kuanzia sasa, ili Watanzania wenye Bongo Tambarare waweze wapate raha ya muziki.
CD hiyo yenye nyimbo tatu zilizojaa ujumbe wenye furaha na mafunzo kwa jamii, kama vile “Supu ya Mawe” ni utunzi na wake kiongozi wa bendi hiyo
kamanda Ras Makunja wa FFU akiimba kwa kushirikiana na mpiga solo
afande Chris-B.
Watanzania tuipokee CD “Bongo Tambarare” na tufurahie Saba Saba kwa
kupata raha ya “Supu ya Mawe” kutoka kwa Kikosi kazi Ngoma Africa aka FFU.
unaweza kusikiliza pia at www.ngoma-africa.com au http://www.ngoma-africa.com