Watano Kushtakiwa kwa Kutoa Siri za Papa

Pope Francis

Pope Francis


WATU watano wamefunguliwa mashtaka Makao Makuu ya Kanisa Katoliki, Vatican kwa tuhuma za kutoa na kuchapisha nakala za siri zinazoonesha usimamizi mbaya katika Ofisi hiyo takatifu. Waandishi wawili waliopata nakala hizo katika vitabu viwili watakabiliwa na kesi hiyo wakiwemo wanachama wawili wa tume ya Papa pamoja na Naibu mmoja.

Iwapo watapatikana na hatia huenda wakahudumia kifungo cha miaka minane jela. Vyombo vya habari vimeshtumu kesi hiyo. Mmoja wa waandishi aliyefunguliwa mashtaka aliitaja hatua hiyo kama uvamizi wa uhuru wa vyombo vya habari.

Waandishi hao Emiliano Fittipaldi na Gianluigi Nuzzi, waliandika kuhusu usimamizi mbaya wa fedha za wahisani katika vitabu vyao vya Merchants in The Temple na Avarice. Madai hayo yanaorodhesha uimarishaji wa makao ya makadinali na mengine.

Watatu hao wanaodaiwa kutoa siri za nakala hizo ni raia wa Uhispania Padri Angelo Lucio Vallejo Balda, Katibu wake na Ofisa mmoja wa mahusiano ya umma anayekaa katika tume inayomshauri papa kuhusu masuala ya mabadiliko ya kiuchumi.
-BBC