Furaha ya kumuona Mh. Lowassa, ilitawala ukumbi mzima |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kulia) akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mkoa wa Njombe, waliofika kwenye Ofisi ya CCM Wilaya ya Njombe Jana, kwa ajili ya kutia saini fomu za kumdhamini ili ateuliwe kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 360.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mkoa wa Iringa, waliofurika kwenye Ofisi ya CCM Wilaya ya Iringa mjini Jana, kwa ajili ya kutia saini fomu za kumdhamini ili ateuliwe kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini 317.
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Steven Wasira akiongea na baadhi ya wanachama wa CCM mkoani Mtwara alipofika kuomba kudhaminiwa
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Steven Wasira akipokewa na baadhi ya wanachama wa CCM mkoani Mtwara alipofika kuomba kudhaminiwa
Na Woinde Shizza
WAZIRI wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Steven Wasira,amewahimiza wakazi wa Mtwara kuwekeza katika uzalishaji wa mazao ya kilimo na uvuvi ikiwa ni sehemu ya shughuli za kiuchumi zitakazowanufaisha kutokana na kugundulika kwa gesi asilia katika ukanda wa kusini mwa nchi.
Wasira ambaye pia ni Mbunge wa Bunda alikuwa akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliomdhamini ili apitishwe na chama hicho kuwania Urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Alisema ingawa zipo fursa nyingi zitakazowanufaika
Watanzania kutokana na sekta hiyo mpya
(gesi), lakini mazao ya kilimo na uvuvi yanaweza kuwa miongoni mwa shughuli
zitakazowanufaisha wananchi wengi hasa wa hali ya chini.
Watanzania kutokana na sekta hiyo mpya
(gesi), lakini mazao ya kilimo na uvuvi yanaweza kuwa miongoni mwa shughuli
zitakazowanufaisha wananchi wengi hasa wa hali ya chini.
Mtwara ni eneo lililowahi kukumbwa na machafuko kutokana
na hisia tofauti zilizokuwapo kuhusu manufaa yanayopaswa kuwafikia wakazi wa
mkoani Mtwara, hasa kuhusu ujenzi wa viwanda na kuibadili gesi ili
itakaposafirishwa isiwe katika mali ghafi.
na hisia tofauti zilizokuwapo kuhusu manufaa yanayopaswa kuwafikia wakazi wa
mkoani Mtwara, hasa kuhusu ujenzi wa viwanda na kuibadili gesi ili
itakaposafirishwa isiwe katika mali ghafi.
Hata hivyo, Wasira alisema anatarajia kufungua fursa
nyingi zaidi za kiuchumi kwa ajili ya wananchi kama atateuliwa na CCM na
hatimaye kushinda katika Uchaguzi huo.
nyingi zaidi za kiuchumi kwa ajili ya wananchi kama atateuliwa na CCM na
hatimaye kushinda katika Uchaguzi huo.
Hakuelezea kwa undani kutokana na kuwa wakati wa kampeni
bado haujafika, bali sasa hivi anatafuta udhamini ndani ya CCM.
bado haujafika, bali sasa hivi anatafuta udhamini ndani ya CCM.
Wakati huo, Wasira na mtia mwingine, Makongoro Nyerere,
wameelezea kuridhika na namna wanavyoshiriki mchakato wa kusaka Urais kwa
kutumia magari, tofauti na watia nia waliowekeza fedha nyingi kiasi cha kutumia
usafiri wa angani katika maeneo mengi.
wameelezea kuridhika na namna wanavyoshiriki mchakato wa kusaka Urais kwa
kutumia magari, tofauti na watia nia waliowekeza fedha nyingi kiasi cha kutumia
usafiri wa angani katika maeneo mengi.
Waliyasema hayo walipokutana kwenye ofisi za CCM mkoa wa
Mtwara, ambapo Makongoro, alirukaruka na kumkumbatia Wasira. Tukio hilo lilitafsiriwa
kuwa ni ishara za umuhimu wa kufanya ushawishi kwa amani pasipo kuiathiri CCM,
wanachama ama Watanzania kwa ujuma.
Mtwara, ambapo Makongoro, alirukaruka na kumkumbatia Wasira. Tukio hilo lilitafsiriwa
kuwa ni ishara za umuhimu wa kufanya ushawishi kwa amani pasipo kuiathiri CCM,
wanachama ama Watanzania kwa ujuma.
“Hizi ndizo siasa tunazozitaka ndani ya CCM na Tanzania
yetyu, sio wagombea wengine wanaotumia utajiri na fedha zao kuwakandamiza
wadogo na kuibua mafarakano kwenye jamii,” akasikika kiongozi mmoja wa CCM
(jina tunalo) akisema.
yetyu, sio wagombea wengine wanaotumia utajiri na fedha zao kuwakandamiza
wadogo na kuibua mafarakano kwenye jamii,” akasikika kiongozi mmoja wa CCM
(jina tunalo) akisema.
Wasira, alikwenda pia katika mkoa wa Lindi ambapo
alifadhiliwa. Leo (alhamis) ataelekea mkoani Mwanza kuendelea na ziara ya
kuomba udhamini kwa wana-CCM wa mikoa ya kanda ya Ziwa Victoria.
alifadhiliwa. Leo (alhamis) ataelekea mkoani Mwanza kuendelea na ziara ya
kuomba udhamini kwa wana-CCM wa mikoa ya kanda ya Ziwa Victoria.