Wasichana 80 wa mimba za utoto wanolewa

Muwezeshaji kutoka asasi ya Poverty Fighting Tanzania, Issa Tunduguru akitoa mada juu ya umihimu wa vicoba kwa wasichana waliopata ujauzito katika umri mdogo (PICHA NA TEYODEN)

JUMLA ya wasichana 80 waliopata mimba katika umri mdogo na kutelekezwa na wanaume kutoka Kata za Azimio, Mtoni, Vijibweni na Kibada wilayani Temeke wamepatiwa mafunzo ya Stadi za Maisha, Ujasiliamali na elimu ya VICOBA kutoka asasi ya ‘Poverty Fighting Tanzania na TEYODEN.

Taarifa hiyo imetolewa jana na Katibu wa TEYODEN, Yusuph Kutegwa alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam. Akifafanua zaidi Kutegwa amesema mafunzo hayo pia yamefadhiliwa Population Council kupitia usimamizi wa Tasisi ya Maendeleo Shirikishi ya Vijana Arusha (TAMASHA).

Alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwa jengea uwezo wasichana jinsi gain ya kuweza kukabiliana na changamoto mabalimbalai za maisha zinazo wazunguka katika maeneo wanayotoka.

“Mafunzo haya yamewafanya wasichana kuondokana na upweke na kuweza kuwapa hali mpya ya kujiamani kuwa wao ni moja sehemu ya jamii na wanweza kufanya mabao mengi zaidi ya walivyo tarajiwa kma wengine ambao wako mashuleni,” alisema Kutegwa.

Aidha aliongeza kuwa mafunzo hayo yamewawezesha wasichana kwenda kuanzisha vikundi vidovidogo vya watu kumi kumi ambavyo vitaweza kuibua miradi ya maendeleo. Pamoja na hayo ameeleza kuwa wasichana hao hawataachwa bure bali watawezeshwa kwa kupatiwa mitaji kutoka TEYODEN kupitia miradi ambayo wameianzisha kwa lengo la kusonga mbele kimaisha.

Temeke Youth Development Network (TEYODEN) ni Mtandao wa Maendeleo ya Vijana unaoendeshwa na vijana wenyewe miongoni mwa mitandao 19 iliyotokana na programu ya vijana nje ya shule iliyotekelezwa na Halmashauri 19 nchini Tanzania kwa ufadhili wa UNICEF. Mtandao umesajiriwa chini ya ofisi ya Makamu wa Raisi, namba ya usajiri ni OONGO/0170.TEYODEN inasimamia na kuratibu shughuli zake katika vituo 24 vya vijana vilivyopo katika kata 24 za Manispaa ya Temeke.

Lengo Kuu la TEYODEN ni kuchangia juhudi za kuleta maendeleo endelevu na thabiti ya tabia na mienendo ya vijana katika mahusiano yao hususani katika masuala ya ngono ili kupunguza kasi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi na kutekeleza mkakati wa kupunguza umasikini ili kufikia malengoya milenia (MDG`s).