WATU hao ambao ni raia wa Kenya na picha zao zilisambazwa kwa umma kabla, walijisalimisha wenyewe kwa wakuu Jumamosi iliopita.
Vita dhidi ya ugaidi nchini Kenya vimekosolewa, huku polisi wakishutumiwa kutokuwa makini katika uchunguzi wao .
Msemaji wa polisi nchini Kenya, Eric Kiraithe aliiambia BBC, kwamba bado wako imara katika kupambana na ugaidi licha ya washukiwa hao kuachiliwa huru.
Na wakati huo huo bomu la kurushwa kwa mkono nchini Kenya lime waua watoto watatu na wengine kujeruhiwa.
Polisi katika jimbo la magharibi la Mount Elgon, walisema inaelekea guruneti hilo liliachwa wakati wa mapigano baina ya jeshi na wapiganaji wa eneo hilo, katika mzozo kuhusu ardhi, mwaka wa 2008.
Jeshi lilisema, guruneti hilo siyo la aina wanayo-tumia.
-BBC