Washiriki Miss Utalii 2012/13 Watembelea Chuo Kikuu cha Uandishi

Mratibu wa Masoko wa Chuo kikuu cha Waandishi wa Habari na Mawasiliano Bi Sophia Akizungumza Jambo na Washiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012/13.


WASHIRIKI wa Shindano la Miss Utalii 2012/13 wametakiwa kutumia elimu zao kutangaza utalii wa Tanzania jambo ambalo litakuwa na manufaa kwao na Taifa kwa jumla. Ushauri huo umetolewa na Mratibu wa Masoko wa Chuo Kikuu cha Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma, Bi. Sophia Ndibalema alipokuwa akizungumza na washiriki hao walipotembelea Chuo hicho jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa masoko wa chuo hicho ndugu Sophia Ndibalema aliwataka kutumia fursa ya kuwa warembo hasa utalii kwa kujitaftia nafasi zaidi za elimu ya juu kwa manufaa yao Jamii na Taifa kwa ujumla, alisema nafasi zipo wazi kwa wale wenye kuhitaji na wenye sifa za kujiunga chuoni hapo kwa nafasi ya Cheti.

Diploma na Shahada, alisema amefurahishwa na muonekano wa asili na mavazi ya heshima kwa washiriki hao hivyo kuondoa dhana kuwa washiriki wa urembo kuwa ni wale wanaovaa mavazi yenye Kudhalilisha jamii hii inathibitisha kuwa Miss Utalii ni Zaidi ya Mashindano Mengine na ni Alama ya Urithi wa Taifa na kielelezo cha mwanamke au Binti wa Kitanzania.