Wasanii waungana kuwanasa Wadurufu wa Kazi zao

Baadhi ya Kazi feki za Wasanii zilizokatwa

Msanii Mohamed’NICE’akilia kwa Uchungu baada kukuta Kazi feki zikiuzwa katika moja ya Maduka

Mtuumiwa wa kudurufu Kazi za Wasanii akiwa chini ya Ulinzi baada ya kukamatwa

Wasanii Mzee Yusufu na Mohamed Nice wakiwa katika Duka lililokamatwa kwa kuuza Kazi feki katika Msako uliofanywa wakishirikiana na Kampuni ya Steps Entertainment

Msemaji wa Kampuni ya Steps Kambarage Ignatios amesema kuwa ukamataji huo si wa zimamoto watahakikisha wanashirikiana na wasanii wenyewe kukamata kazi zao maana wasanii wengi wanadai kuwa kazi zao zinatoka sana kumbe zinachakachuliwa na kuwapa faida watu ambao wanakaa tu na kusubili kazi za wasanii ameiomba serikali kuchukua atua kali ili iwe fundisho kwa watu wanaorudufu na kunyonya kazi za wasanii hawo

Na mmoja ya wasanii waliojitokeza katika kamatakamata hiyo iliyofanyika makutano ya mtaa wa Magila na Likoma Kariakoo, Msanii Mohamedi Nice ‘Mtunisi’ amesema watu hawa wana akili za ziada kwani katika kava ya mbele wanaweka stika yetu halali na DVD ndio inakuwa imechakachuliwa akiangua kilio na kusema wasanii wakifa wanakufa masikini kumbe ni watu wachache ndio wamekuwa wakinufaika na kazi zao bila kushiriki chochote

Baadhi ya wasanii walioshiriki katika kamatakamata hiyo ni pamoja na Jacobo Stevin ‘JB’, Mzee Yusuph wa kundi la Taarabu la Jahazi, Simoni Mwapagata (Rado), Mussa Msuba wa iliyokuwa Segere Orginal, Seles Mapunda ,Mohamed Nice ‘Mtunisi’ na wengine wengi wasanii hao wameungana pamoja kwa ajili ya kutetea kazi zao ili zisirudufiwe kiolela na kuiomba serikali kupitisha sheria kali kwa mtu anaekamatwa na kazi kama hizo zilizokamatwa

Na Rajabu Mhamila