Wasanii wakubwa wanauwa muziki wa Bongo

Baadhi ya viongozi waandaaji wa Kili Muzic Award

TULITEGEMEA wasanii wakubwa kama Ambwene Yesaya (A.Y) kama anavyofaamika zaidi kwa mashabiki wengi wa muziki, angekuwa ni mfano wa kuigwa na wanamuziki chipukizi nchini, ila badala yake ameonekana kuwa kikwazo kikubwa cha kukua kwa muziki wa rege (reggae) hapa Tanzania.

Sisi kama Jahson na Susu hatuwezi kujifunza lolote kutoka kwa msanii huyo (A.Y) kwa sababu amekuwa ni mtu alionesha kuingilia muziki wa staili nyingine kwa hali ya juu mara kadhaa mfano.

Wengi tunamjua A.Y kama msanii wa hip hop lakini mwaka 2010 aliwai kushindania tunzo ya mwanamuziki bora wa reggae na hatimaye kupata tunzo hiyo na kuichukua kwa mbwebwe zote. Pia mwaka 2012 amewekwa kwenye categori ya ragga na nina imani atapata tu tunzo hiyo kutokana na udhaifu uliopo katika uandaaji wa tunzo hizo za Kilimanjaro Music Award.
Bushoke alikuwa mfano mzuri sana wa kuigwa alipopewa tunzo ambayo hakustahili na kuikataa je A.Y kwanini alikubali tunzo hiyo? Na ki ukweli haikumstahili.

Ki ukweli wasanii kama A.Y wanatuvunja moyo sana sisi wasanii ambao tunaofanya muziki huo pamoja na mashabiki wa muziki huo wa reggae na ragga. Kiukweli A.Y asijidanganye kwamba wingi wa kura zake katika kinyang’anyiro hicho, zinatokana na mashabiki wa Reggae na ragga, no huo ni uongo bali ni mashabiki wake wa hip hop ndo wanaomuwezesha. Kwa hiyo binafsi tunaona anawakanganya wapenzi hao.

Sisi kama washikadau wakubwa wa muziki wa Ragga na Reggae tunasikitishwa sana kwa upungufu mkubwa wa uzalendo wa msanii A.Y kuzidi kukumbatia udanganyifu wa sifa unaofanyika kila mwaka, sijui anatufundisha nini wasanii chipukizi.

Kimsingi hatutoi maoni kwa kuonesha chuki kwa A.Y, ila tunajalibu kuweka mambo wazi na kutoruhusu udanganyifu huu kuendelea kwenye vyombo husika maana kunawakati wengine. Na hali hii ikiachwa ipo siku watu wa aina hii wanaweza kuimba hata taarabu na bolingo na kuingizwa kwenye categori hiyo na kuchukuwa.

Inawezekana kabisa akawa anauwa muziki wake ama anawagawanya mashabiki wake kwa kutotulia kwenye mtindo wa aina moja wa muziki wake kama ilivyo kwa wasanii wengine. Tungependa washikadau wakubwa wa muziki huu walione kama hili ni tatizo na walikemee kwa nguvu zote ili Tanzania iwe na ukomavu wa muziki huu tofauti na kile kupiga kwata bila kusonga mbele.

Mfano sisi tumeshafanya nyimbo kama Heat na Show me some love ambazo zimefanya vema katika vituo mbalimbali lakini tumeenguliwa kwenye tunzo hizo jambo ambalo linakatisha tamaa sana, lakini tutaendelea kupambana. Tunaamini mashabiki wanaelewa kuwa tunafanya vema kabisa japo kuna wasanii wengi wakali waliamua kuachana na muziki kutokana na mambo ya kukatisha tamaa kama haya.

Wapenzi wa muziki jaribu kuingia kwenye youtube na msearch Jahson & Susu ama Jahson Tanzania mnaweza kutoa maoni yenu, kwamba tunastahili tunzo au lah?
Asanteni: By Jahson na Susu