Wasanii wa Tanzania Uingereza Wakutana na Balozi Asha Migiro

Balozi Migiro na mwanamuziki Msafiri a.k.a Diouf Lewandowski

Balozi Migiro na mwanamuziki Msafiri a.k.a Diouf Lewandowski.

Picha ya pamoja. Kutoka kushoto , Rama Sax – aliyekuwa bendi ya Simba wa Nyika zamani, Saidi Kanda aliyepiga na marehemu Remmy Ongala, Hamida Mbaga wa All Things African, Khadija Ismail wa Kibisa na Muungano ya enzi hizo, Balozi Dk Asha Rose Migiro, Neema Kitilya anayetangaza mapishi ya Kitanzania Ungereza na Msafiri anayetumia jina la Diouf Lewandowski. Waliochuchumaa mbele ni Freddy Macha na Fab Moses

KUNDI la wasanii wanane waliwakilisha wenzao wakazi Uingereza Jumatano iliyopita katika kikao na Balozi mpya wa Tanzania nchini humo, Dk. Asha Rose Migiro.
Kikao hicho kilichoitwa na mheshimiwa Balozi kilikuwa na madhumuni ya kuweka ushirikiano kati ya jumuiya ya wasanii na Watanzania na Ubalozi wetu. Balozi Migiro alisisitiza kuwa sera ya awamu ya tano ni kuipa sanaa kipaumbele ili kuchangia maendeleo yetu ndani na nje.
Wasanii hao walioongozwa na mcheza sarakasi na mwanamuziki Fab Moses walijitolea bila malipo yeyote – wengine kutoka safari za mbali sana.
WASATU – Wasanii Tanzania Uingereza- ilisisitiza haja ya kujituma zaidi kujenga sanaa na mawasiliano na kusaidiana kujuana kuendeleza fani hii muhimu.

Balozi Migiro na mtangazaji bidhaa na mavazi ya Kitanzania, Hamida Mbaga

Balozi Migiro na mtangazaji bidhaa na mavazi ya Kitanzania, Hamida Mbaga