
Waandishi wa habari za michezo pamoja na wasanii, wakitembea kwenda kuangalia ujenzi unaoendelea wa nyumba zao, katika kijiji cha Mwanzega Kimbiji Tarafa ya Mkuranga Chingungweni Mkoa wa Pwani jana kutoka kulia ni Tomm Chilala, Kibwana Dachi na Kikumbi Mwanza Mpango 'King Kiki'.

Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA), Cassim Taalib (katikati) akimwelekeza Sheikh Majaliwa Selemani aliekwenda kuangalia maendeleo ya Kijiji cha Mwanzega Mkulanga Tarafa yaChingungweni, zinapojengwa nyumba kwa ajili ya wasanii, Sheikh Majaliwa, alitoa ahadi ya kujenga Msikiti na Madrasa itakayofadhiliwa na African Relief Comettee Kuwait.