Warusi waonesha nia kuwekeza Tanzania

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt Shaaban Mwinjaka amewataka wawekezaji wenye nia njema kuja nchini na kushirikiana na wazalendo katika kutumia fursa mbali mbali zilizopo nchini kwa faida na maendeleo ya pande zote mbili.

Dkt Mwinjaka ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam, katika mazungumzo mafupi kati yake na ujumbe wa wawekezaji kutoka nchini Urusi wenye nia ya kuwekeza nchini Tanzania.
Ujumbe huo wa Wawekezaji kutoka Urusi umeongozwa na Bw Aundrey Brazhnik umekuja nchini ili kufanya mazungumzo na mamlaka mbali mbali kwa lengo la kuwekeza katika miradi ya kuzalisha nishati ya Umeme na uchimbaji wa madini ya aina mbali mbali.

‘Wizara yangu inapenda kuwakaribisha wawekezaji kuja nchini mwetu kushirikiana na Watanzania, tutawapa ushirikiamno wa kutosha ili sote tufaidike na uwekezaji wao ili Taifa na wananchi wake, tufaidike kupitia fursa mbali mbali.’ Amesem,a Dkt Mwinjaka.