
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa akisalimia na Msimamizi (Matron) wa warembo wa Redd’s Miss Tanzania 2012, Irene Karugaba wakati Warembo hao walipotembelea Nyumbani kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Monduli ili Kupata Baraka zake. Lowassa aliwapokea warembo hao kwa furaha na kuzungumza nao machache juu ya mafanikio ya Mashindano hayo na Maendeleo ya Taifa letu la Tanzania.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa akizungumza na Warembo wanaowania Taji la Redd’s Miss Tanzania 2012 waliofika nyumbani kwake Monduli na kupata wasaa kwa kuzungumza nae mambo mawili matatu juu ya mafanikio ya Mashindano hayo na Maendeleo ya Taifa letu kwa ujumla.