Bango la ofisi ya wakala wa Usafiri wa Haraka (DART) lililoko Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.
Msimamizi wa mradi huo, akitoa maelezo kwa warembo wa Redd’s Miss Kinondoni 2013 ambao waliambatana na Madiwani wa Viti Maalum kutembelea ofisi ya wakala wa Usafiri wa Haraka zilizoko Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam. Ziara ya warembo hao ilikuwa na nia ya kuwajengea uwezo warembo hao waweze kutambua miradi mbali mbali inayoendeshwa na serikali.
Warembo wa Redd’s Miss Kinondoni 2013 wakimsikiliza Kaimu Mtedaji Mkuu wa ofisi ya wakala wa Usafiri wa Haraka (DART), Bi. Astelia Mrambo mara baada ya kutembelea ofisi kwake.
Kaimu Mtedaji Mkuu wa ofisi ya wakala wa Usafiri wa Haraka (DART), Bi. Astelia Mrambo akiwa na mratibu wa shindano la Redd’s Miss Kinondoni 2013 wakiwaongoza warembo kuangalia ujenzi wa vituo vya mabasi yaendayo kwa haraka kituo hicho kilichokatika hatua za mwisho kukamilika kipo Manzese jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mtedaji Mkuu wa ofisi ya wakala wa Usafiri wa Haraka (DART), Bi. Astelia Mrambo akiendelea kutoa ufafanuzi juu ya mradi huo.
Maelezo yakiendelea kutolewa…
Kaimu Mtedaji Mkuu wa ofisi ya wakala wa Usafiri wa Haraka (DART), Bi. Astelia Mrambo akifanya mahojiano na vyombo ya habari.
Mshiriki wa Redd’s Miss Kinondoni 2013 akieleza machache waliyojifunza.
Mashindano ya Redd’s Miss Kinondoni yanatarajiwa kufanyika June 21, huku walowa yamedhaminiwa na Redd’s Original, Chilly Willy Energy Drink, Oriflame Natural Beauty Products, Times Fm, JB Belmonte Hotel, Michuzi Media Group, Michuzijr Blog, Mtaa Kwa Mtaa Blog, Fullshangwe Blog, Mroki Blog, Sufian Mafoto Blog, Global Publisher, Mdimuz Blog, Lukaza Blog, MO Blog, Dj Choka Blog na Kajunason Blog.