Wapiganaji wa CAR wasonga mbele


Wapiganaji katika Jamhuri ya Afrika ya Kati wameuteka mji wa Bambari, mji wa tatu kwa ukubwa.
Huo ni mji wa sita kutekwa na wapiganaji hao tangu kuanza kupigana awali mwezi huu, na ndio karibu kabisa na mji mkuu, Bangui, kwa wapiganaji hao kuwahi kufika.
Msemaji wa shirika la msaada wa matibabu, Medecins Sans Frontieres, ameeleza kuwa watu wengi wamekimbia makwao kwa sababu ya mapigano, pamoja na yale maeneo ambayo bado yanadhibitiwa na jeshi la serikali.
Wapiganaji hao – wanaoitwa ushirikiano wa Seleca – wanataka kumtoa madarakani Rais Francois Bozize ambaye wanamshutumu kuwa hakutimiza ahadi za mkataba wa amani.

-BBC