
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Tulia Ackson kizungumza wakati wa kutoa baraka kwa wanaharakati 89 wakiwemo wafanyakazi wa Kampuni ya Acacia wanaoshiriki zoezi panda mlima kwa lengo lakuchangisha fedha kwa ajili ya mapambano, vita dhidi ya Ukimwi.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Tulia Ackson akitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika lango la kupandia mlima Kilimanjaro, lango la Machame kwa ajili ya kutoa Baraka kwa washiriki wa changamoto ya kupanda mlima kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi zoezi linaloratibiwa na Kampuni ya Geita Gold Mining (GGM).
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Geita Gold Mining (GGM) Terry Melpeter akizungumza katika shughuli hiyo iliyofanyika katika lango la Machame.
Baadhi ya viongozi wa wilaya za Hai na Moshi mjini wakifuatalia shughuli hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro mshikizi Mrisho Gambo akizungumza wakati wa shuguli hiyo ambayo hufanyika kila mwaka.
Zoezi la kuapnda Mlima likianza rasi huku likiongozwa na Naibu Spika, Dkt Tulia Ackson, Mrisho Mpoto akiongoza kwa nyimbo za kuhamasisha.