Marekani.
UTAFITI uliofanywa hivi karibuni umeonesha kuwa wanawake wanaovuta sigara wapo hatarini kuliko wanaume wavutaji wa ulevi huo. Wanawake wapo hatarini kushambuliwa na maradhi ya moyo zaidi wanaume walio na kiu ya uvutaji.
Utafiti ulioendeshwa miongoni kwa zaidi ya watu milioni 2, umebaini wanawake wako kwenye hatari ya maradhi ya moyo kwa asilimia 25 wakati wanapotumia tumbaku hiyo.
Hata hivyo, sababu za matokeo haya hazijatolowa japo watafiti kutoka Marekani wamesema wanawake wako kwenye hatari kubwa ya kuvuta kemikali zenye simu kutoka kwa sigara ikilinganishwa na wanaume.
Hali hiyo wameongeza imejitokeza katika idadi ya wanawake wanaopata saratani ya mapafu ikilinganishwa na wanaume wanaovuta sigara.
-BBC