Wanawake Wataka Katiba Mpya Itamke Umri wa Kuolewa, Kuoa

Mmoja wa wanawake akichangia mada katika mjadala wa wazi uliofanyika mjini Dodoma.

Mmoja wa wanawake akichangia mada katika mjadala wa wazi uliofanyika mjini Dodoma.

Maandamano wanawake wakidai haki mbalimbali za kijinsia ziingizwe katika katiba inayoandaliwa mjini Dodoma.

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

WANAHARAKATI wanaoshiriki kongamano la Katiba la kujadili masuala ya kijinsia yanayotakiwa kuzingatiwa kwenye mjadala wa Bunge maalum la Katiba wamewataka wajumbe wa Bunge maalum la Katiba kuhakikisha katiba mpya itakayotengenezwa inatamka umri wa kuolewa au kuoa uwe miaka 18 hadi 21 ili kuwapa nafasi watoto wa kike kupata nafasi ya kusoma na kukua.

Wakizungumza wakati wakiendesha Bunge kivuli au Bunge maalum maalum la Katiba lililoandaliwa na TGNP Mtandao kwa kushirkiana na Mtandao wa Wanawake na katiba mjini Dodoma, wanaharakati hao wamesema kuwa wajumbe wa Bunge maalum bila kujali tofauti zao za kijinsi wanapaswa kuhakikisha wanapigania haki ya mtoto wa kike kuwa salama na kutokuolewa kabla ya kukomaa akiwa na umri wa chini ya miaka 18.

Akizungumza Mwenyekiti wa Bunge maalum Mbadala la Katiba Dk. Vicensia Shule amesema kuwa wananchi wote wanatakiwa kuunganisha nguvu wakati huu wa mchakato wa Bunge la Katiba kuhakikisha masuala muhimu ya wanawake na yale ambayo yanatoa ulinzi kwa makundi yaliyoko pembezoni yanazingatiwa na kuingizwa kwenye katiba mpya.

“hakuna taifa ambalo ni tajiri au watu wake wameendelea bila kupata elimu, na kuzingatia usawa wa kijinsia. Haya yote yatafanyika kama kuna elimu ya kutosha kwa wasichana na kama wataolewa  wakiwa watoto hawataweza kupata elimu,” alisema Dk. Shule.

Mshiriki kutoka shirika la Active Youth of Tanzania Mwanza, Amina Kisero alisema kuwa sheria ya ndoa ya mwaka 1971, imeelza kuwa umri wa kuolewa kwa msichana ni miaka 14 au 15 wakati kanuni ya adhabu siura ya sita sheria za Tanzania namba 1 na 2(i) kinaahalalisha kitendo cha ubakaji kwa kigezo cha kuolewa.

“Vipengele vyote hivi ni kikwazo kwa mustakabali wa ulinzi  wa haki za mtoto, na haki ya afya ya uzazi kwa mujibu wa sheria ya mtoto ya mwaka 2009, tunataka kama katiba mpya itatambua na kuweka bayana juu ya ulinzi wa mtoto wa kike sheria hizi zitafungwa,” alisema Kisero.

Kwa upande wake Khadija Haddy ambaye pia ni mtaalam wa afya ya Jamii kutoka YAP alisema kuwa mtoto wa kike mwenye umri wa chini ya miaka 18 maumbile yake hayana uwezo wa kupokea mabadiliko ya kubeba ujauzito na kuzaa kwa wakati unaotakiwa. Alisema kuwa ndo za utotoni zinasababisha tatizo kubwa la kuongezeka kwa magonjwa ya wanawake kutokana na maumbile yao kushindwa kubeba mabadiliko ya kimwili.

Kwa mujibu wa takwimu ya UNFPA za mwaka 2013 tatizo la ndo za utotoni linakuwa kwa kasi nchini licha ya kampeni kubwa ya wananchi inayopigwa kupambana na hali hiyo. Wilaya ya Shinyanga ikiongoza kwa asilimia 59, Tabora asilimia 58, Mara asilimia 55, Dodoma asilimia 51 na lindi asilimia 45. Kongamano hili linaandaliwa na Mtandao wa Wanawake na Katiba kwa kushirikiana na TGNP Mtandao mjini Dodoma na kuwashirikisha wanawake na wanaume na makundi yote ya kijamii zaidi ya 200 na wajumbe wa Bunge maalum la Katiba.