WANAWAKE kutoka mikoa yote nchini wamepata fursa ya kushiriki Kongamano la kwanza la Kitaifa la wanawake kujadili masuala muhimu ya haki za wanwake wanazotaka ziingie kwenye Katiba mpya.
Kongamano hilo liloandaliwa na Mfuko wa Wanawake Tanzania (WFT), linafanyika kwa siku tatu kuanzia 22-24 Oktoba 2012 jijini Dar es salaam, ambap[o watajadili kwa kina na kuchambua mapungufu ya katiba inayotumika hivi sasa na kuwekeana maazimio ya masuala yatakayotakiwa kuingizwa kwenye mahudhui ya Katiba mpya inayotarajiwa kuanza kutumika ifikapo 2014.
Pamoja na mambo mengine, mada zinazotolewa kwenye Kongamano hilo ni Umuhimu wa katiba katika maendeleo ya wanawake, mapungufu ya Kijinsia Katika Katiba iliyopo, haki za msingi za mwanamke za kuzingatia Katika katiba mpya, masuala muhimu ya kuzingatia katika haki za wanawake na kuwekeana mikakati ya kutumia vizuri fursa ya mchakato wa uuandwaji wa katiba mpya.