Somalia,
UMOJA wa Mataifa (UN) umearifu kwamba wanawake wanaoikimbia njaa Somalia wanazidi kuwamo katika hatari ya kufanyiwa vitendo vya ngono kwa mabavu, wanapokuwa njiani kuelekea kwenye kambi ya wakimbizi nchini Kenya.
Wakati jumuiya ya kimataifa inaimirisha juhudi za kuyaokoa maisha ya mamiloni ya wasomali waliomo katika hatari ya kufa njaa, wanawake wa nchi hiyo wanaoikimbia njaa nchini mwao wanakuwamo katika hatari nyingine.
Umoja wa Mataifa umearifu kwamba wanawake hao wanazidi kufanyiwa vitendo vya ngono kwa mabavu wanapokuwa njiani kuelekea nchini Kenya.
Wanawake wa KisomaliMjumbe maalamu wa Umoja wa Mataifa bibi Margot Wallström anaepambana na uhalifu wa vitendo vya ngono ya mabavu amesema hali ni ya kutia wasiwasi mkubwa.
Wallström amesema wakati wanawake na wasichana wa kisomali wanapokuwa njiani wakitembea kwa muda mrefu ili kufika kwenye kambi za nchini Kenya, wanashambuliwa na kubakwa na wanamgambo na wahalifu.
Mjumbe huyo maalum wa Umoja wa Mataifa bibi Wallström amesema taarifa za kutisha zinawasilishwa kwenye ofisi yake juu ya wanawake wanaobakwa pia na askari wa Serikali ya mpito ya Somalia.
Mjumbe huyo pia amefahamisha kwamba wasichana wanatekwa nyara na kulazimishwa kuolewa na wapiganaji wa kundi la waislamu wenye itikadi kali Al Shabaab. Bibi Wallström ametoa mwito wa kuchukua hatua za kuyakomesha mazingira hayo ya kukiukwa haki za binadamu.
Wakati huo huo ameipongeza Serikali ya Kenya kwa kuwakubali maalfu ya wakimbizi wa kisomali na kuwapa hifadhi nchini.
Na taarifa kutoka Nairobi zinasema mashirika ya misaada yanapeleka mahitaji ili kuwasaidia mamilioni ya watu kwenye eneo la pembe ya Afrika waliomo katika hatari ya kufa njaa.
Hali hiyo imesababishwa na mavuno hafifu kutokana na ukame ambao haujawahi kuonekana katika Pembe ya Afrika katika kipindi cha miaka sitini iliyopita.
Tatizo linatokea ikiwa nchi zinazokumbwa na maafa ya ukame hazina akiba ya fedha za kigeni ili kuweza kununua chakula kwenye masoko ya dunia.”
Profesa Von Witzke ameeleza kuwa maafa ya Somalia yangeliweza kuepushwa laiti wakulima wadogo wadogo wangelipatiwa utaalamu wa kisasa ilikweza kuongeza uzalishaji.
Profesa huyo pia amesema kurudi nyuma kwa harakati za utafiti wa kilimo duniani pia kumechangia katika maafa ya njaa kwenye pembe ya Afrika. Ameeleza kuwa matokeo yake ni kupungua uzalishaji na kuongezeka bei ya vyakula.