Mwenyekiti wa Muungano wa Wanawake wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (MMPT) Misheni ya Kijitonyama, Maines Mhama (kulia), akimkabidhi maua mgeni rasmi wa maadhimisho ya siku ya wanawake wa kanisa hilo, Anitha Mshighati (katikati), mara baada ya kuwasili kwenye sherehe hiyo iliyofanyika Kanisa la Pentekoste la Kituo cha Tabata Kisiwani Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mchungaji Ibrahim Mshighati mume wa mgeni rasmi.
Hapa ni furaha tupu wakati mgeni rasmi akisindikizwa kuingia kanisani.
|
Mgeni rasmi Anitha Mshighati akizungumza katika maadhimisho hayo.
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Pentekoste Kituo cha Tabata Kisiwani, John Shusho akiwa kwenye maombi wakati wa maadhimisho hayo.
Kwaya ya Kanisa hilo Kituo cha Tabata Kisiwani ikitumbuiza
Nyimbo za kusifu zikiendelea.
Kwaya ya Tabata Kisiwani ikiimba.
Kwaya ya Kijitonyama ikiimba.
Kwaya ya Gongo la Mboto ikifanya vitu vyake
Kwaya ya Kipawa haikuwa nyuma kutoa burudani
Mwimbaji wa nyimbo za injili wa kujitegemea, Joyce Agato akiwajibika
Mwenyekiti wa Muungano wa Wanawake wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (MMPT) Misheni ya Kijitonyama, Maines Mhama (kushoto), akiwa na wageni wake mgeni rasmi na mumewe.
Ibada ikiendelea.
Ni kuimba nyimbo za kusifu na kucheza.
Mwenyekiti wa Wanawake Maines Mhama akitoa neno la maadhimisho hayo.
Katibu Msaidizi wa Wanawake wa Kanisla hilo, Joyce Agato akimkabidhi risala mgeni rasmi.
Na Dotto Mwaibale
WANAWAKE wametakiwa kuwa chachu ya kujenga amani nchini badala ya kusubiri iharibike.
Mwito huo umetolewa Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na Mwenyekiti wa Muungano wa Wanawake wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (MMPT) Misheni ya Kijitonyama, Maines Mhama wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake kwa kanisa hilo.
“Wanawake tunapaswa kuwa wa kwanza kujenga amani ya nchi kuanzia kwenye familia zetu kwani inapokosekana waathirika wakubwa ni sisi na watoto wetu” alisema Mhama.
Alisema amani inapokoseka shughuli zote haziwezi kufanyika nchini ikiwa pamoja na kuabudu hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuitunza kwani inapopotea gharama ya kuirudisha inakuwa kubwa.
Akiongelea matukio yanayotokea nchini ya watu kuuana kama yaliyotokea Kibiti mkoani Pwani kwa askari nane kuuana alisema wanadamu wanapaswa kumrudia mungu bila kujali itikadi za dini.
“Matukio ya kuuana yaliyoibuka hivi karibuni yatakwisha kwa watu kuwa na hofu ya mungu na si vinginevyo” alisema Mhama.
Mgeni rasmi kwenye sherehe hizo, Anitha Mshighati aliwataka wanawake kuungana katika masuala mbalimbali na kuanzisha shughuli za ujasiriamali ili waweze kujikomboa kiuchumi.
“Wanawake serikali imetuwekea miundombinu mizuri ya kufanya shughuli zetu tutumie fursa hiyo kujianzishia miradi mbalimbali ili tuweze kufanya mambo makubwa ya kiuchumi” alisema Mshighati.
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni kuitafuta amani na kuidumisha.