Wanaonunua Bidhaa Halisi Waendelea Kufaidika na Promosheni ya Pambika na Samsung

Kutoka kulia ni Bw. Humudi Abdulhussein toka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, katikati ni Mratibu wa promosheni ya Pambika na Samsung Bw. Lawrence Andrew na Chacha Magege wakifuatilia droo kwa makini wakati wa kuchezesha droo ya Pambika na Samsung.

Mratibu wa promosheni ya Pambika na Samsung Bw. Lawrence Andrew akijadiliana jambo na Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Bw. Humudi Abdulhussein Wakati wa kuchezesha droo ya tatu ya Pambika na Samsung mapema hii leo. Zawadi kubwa kabisa ya wiki hii ilikuwa ni Jokofu lenye dhamana ya miaka 10 ambapo mshindi wake ni Bi.  Bernadeta Peter mkazi wa Dar es Salaam huku Bi. Anthonia Julius Masele (45) ambae amejinyakulia luninga ya LED ya Samsung ya inchi 32 wa Dodoma. Hamad Abdallah Hemedi wa Dar es Salaam ambae amejinyakulia kompyuta mpakato.

PROMOSHENI kubwa Samsung inayojulikana kama Pambika na Samsung imefikia wiki ya tatu baada ya kutangazwa washindi 15 wengine na kufanya idadi ya watu 45 kuwa washindi wa droo za kila wiki katika promosheni hiyo tangu kuanza kwake rasmi Novemba 7, 2013. Kama ilivyokuwa kwa droo zilizopita, washindi wa wiki hii pia watakabidhiwa zawadi zao toka Samsung katika hafla maalum ya kugawa zawadi kwa washindi wa kila wiki inayofanyika Jumatano ya wiki hii.

Akizungumza wakati wa droo hiyo ya tatu ya Pambika na Samsung Bw. Sylvester Manyara, Meneja Mauzo na Usambazaji wa Samsung Tanzania amesema kuwa promosheni hii mpaka sasa inaonyesha mafanikio baada ya kuongezeka kwa utamaduni wa kununua bidhaa halisi katika jamii ya Watanzania lakini pia ufahamu juu ya faida za huduma ya dhamana nao umeongezeka. Aliendelea kusema kuwa kuna ongezeko la wateja wapya pia kutembelea maduka ya Samsung kila wiki na hivyo kuonyesha matokeo chanya ya kuelimisha na kuhamasisha Watanzania kupitia kampeni ya Pambika na Samsung.

Akizungumzia jinsi gani Samsung inaendelea kuwaneemesha Watanzania kupitia kampeni yake hii Bw. Manyara alisema kuwa “Kadri tunavyoendelea kubadilisha maisha ya Watanzania, Samsung inajivunia kuwa mstari wa mbele kubadilisha maisha ya kila mmoja kupitia bidhaa zetu zinazokidhi haja ya kila mtu, kupitia Pambika na Samsung tunaendelea na ahadi yetu ya si tu kutoa bidhaa bora na imara bali pia tunatoa nafasi ya kubadilisha maisha ya mtu na kuwa bora zaidi kama hivi tunavyofanya hii leo”

“Samsung kama kampuni bado inaendelea kuimarika kutokana na mapenzi mema tunayoyapata toka kwa wateja wetu. Bado kila siku tunajisikia kwa jitihada zote kuonyesha faraja yetu na kuwazawadia wateja wetu kwa kadri tunavyoweza. Kama sehemu ya kuhamasisha Watanzania kununua bidhaa halisi na kuisajili katika huduma yetu maalum ya dhamana ya miezi 24, Pambika na Samsung ni njia moja wapo ya kuonyesha mapenzi yetu kwa wateja kwa kununua bidhaa halisi za Samsung” aliendelea Bw. Manyara.

Washindi 15 walipataikana katika droo hiyo ambapo baadhi ya washindi walikuwa ni Issa Richard Moshi (23), wa Kilimanjaro aliyejishindia deki ya DVD, Agnes John Mkalango (30) wa Mwanza, Adagoti Komba (57) wa Dodoma, Faustine Kirusya (45) mkazi wa Mbeya ambae ni askari polisi pamoja na Praygod Amos (39) wa Arusha wote wameshinda Muziki wa Nyumbani. Zawadi kubwa kabisa ya wiki hii ilikuwa ni Jokofu lenye dhamana ya miaka 10 ambapo mshindi wake ni Bi. Bernadeta Peter mkazi wa Dar es Salaam huku Bi. Anthonia Julius Masele (45) ambae amejinyakulia luninga ya LED ya Samsung ya inchi 32 wa Dodoma.

Droo hii ya tatu nayo imetoa washindi toka sehemu mbalimbali za nchi ambapo inaonyesha malengo ya kampeni hii kuweza kuwafikia Watanzania wote. Mwanza, Arusha, Mbeya Dodoma, Morogoro, Tabora, Manyara and Dar es salaam ni mikoa iliyotoa washindi wa Pambika na Samsung tangu kuanza kwa droo hii. Promosheni hii inalengo la kuwazawadia wateja ambao wananunua bidhaa halisi kuanzia simu mpaka bidhaa za nyumbani, bado ina wiki tatu zaidi kabla ya zawadi ya mwisho ya gari aina ya Mitsubishi Double Cabin mpya kutolewa Desemba 23, 2013.

Kuingia kwenye mchakato wa kushinda, mteja atatakiwa kununua simu yoyote halisi ya Samsung na kuisajili kwenye huduma Maalum ya ‘E-Warranty’ kwa kutuma namba 15 za utambulisho wa simu yake yaani ‘IMEI’ kwenda namba 15685. Na kwa yule atakaenunua bidhaa nyingine ya Samsung anatakiwa kujaza fomu Maalum inayopatikana katika maduka yote ya Samsung na kwa mawakala waliosajiliwa waliopo nchi nzima na kujihakikishia nafasi ya kushinda katika droo za kila wiki na ile ya mwisho.