Wanaodaiwa na HELSB Sasa Kuweza Kulipa kwa M-Pesa

Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawsiliano toka Bodi ya Mikopo  ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Cosmas Mwaisobwa (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu idadi ya wanafunzi walionufaika na mikopo, ambapo kufikia mwaka 2013 wanafunzi 97,348 walikuwa wamenufaika na mikopo ya bodi hiyo. Kulia ni Ofisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo,  Frank Mvungi na kushoto ni Ofisa Habari Mwandamizi toka bodi, Veneranda Malima.

Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano toka Bodi ya Mikopo  ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Bw. Cosmas Mwaisobwa akifafanua kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu utaratibu mpya wa wanafunzi walionufaika na mikopo ya HELSB  kurejesha mikopo yao kwa njia ya mtandao kuanzia mwezi septemba 2013, ambapo  huduma ya M-Mpesa ilianza kutumika  na kuanzia April 2014, Aitel Money itatumika pia kama mfumo wa kurejesha mikopo hiyo. Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Frank Mvungi.

Frank Mvungi – Maelezo

BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HELSB) imeanzisha utaratibu mpya wa kurejesha mikopo kwa njia ya kutumia mtandao. Hayo yamesemwa leo jijini Das es Salaam na Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa bodi hiyo, Cosmas Mwaisobwa wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

Akifafanua Mwaisobwa alisema kuanzia mwezi Septemba, 2013 Bodi ilianzisha utaratibu mpya wa kurejesha mikopo yao kupitia huduma ya M-Pesa. Mwaisobwa alisema katika kuimarisha mfumo wa urejeshaji mikopo kuanzia mwezi Aprili, 2014 walionufaika na mikopo hiyo wataweza kurejesha kupitia pia kwa mtandao wa Airtel Money.

Alisema hata hivyo kabla ya muhusika kuanza kutumia huduma ya M-pesa, mnufaika wa mkopo anapaswa kuwasiliana na HELSB ili kupata mambo muhimu ambayo ni Taarifa ya Mkopo, (Loan statement) Kiwango cha marejesho, (Loan instalments) na Namba ya kumbukumbu (Loan number).

HELSB pia hutoa msaada kwa waombaji wa mikopo wanaopata matatizo madogo madogo wakati wa kujaza fomu kwa kutumia dawati maalum la msaada kwa wateja ambapo msaada huo hutolewa kwa njia ya simu siku za Jumatatu hadi Jjumaa kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa 2 usiku.

Mwaisobwa alibainisha kuwa baadhi ya changamoto zinazoikabili HELSB ni imani potofu iliyoenea kwamba mikopo hiyo ni ruzuku na ushirikiano hafifu na baadhi ya waajiri katika urejeshaji mikopo.
Mwaisobwa alitoa wito kwa wale wote walionufaika na mikopo kurejesha mikopo hiyo kwa wakati ili kutoa fursa kwa wahitaji wengine kukopeshwa.

“…Tangu kuasisiwa kwake, Bodi hiyo imefanikiwa kutoa mikopo kwa idadi kubwa ya wanafunzi ikilinganishwa na hali ilivyokuwa kabla bodi kuanzishwa, ambapo wanafunzi wameongezeka kutoka wanafunzi 42,729 mwaka 2005/2006 hadi wanafunzi 97,348 mwaka 2012/2013, ongezeko hili ni sawa na wastani wa 10.4% kwa mwaka,” alisema.