Wananchi Wamzomea Ofisa Mipango Miji Mkutanoni

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama.

Na Mwandishi Wetu, Moshi

WANANCHI wa Kijiji cha Uchira Halmashauri ya Moshi mkoani Kilimanjaro wamemzomea Ofisa Mipango Miji wa Halmashauri hiyo kwenye mkutano wa kijiji ambao ulikuwa kwa ajili ya  kuwataka wananchi wabariki mchoro wa mipango miji wa kijiji hicho kuwa mji mdogo.

Mkutano huo ulianza saa tano na nusu na kudumu kwa saa moja kwa malumbano na kupelekea kuvunjika kwa mkutano huo, ambapo wananchi walipinga kijiji hicho kuwa mji mdogo. Wananchi hao walisema kijiji hicho kina kila kitu cha maendeleo zikiwamo shule zahanati kituo cha polisi na mahitaji mengene na kwamba hawahitaji kiwe mji kutokana na kwamba wanategemea kilimo zaidi.

Mmoja wa wananchi hao, Sofia Njau alisema hawataki kijiji hicho kiwe mji kutokana na kwamba, wamekuwa wakitegemea kilimo kwa miaka yote na endapo kijiji hicho kitakuwa mji watanyanganywa mashamba yao na halmashauri.

“Sisi tutakapo kubali hapa pawe mji tunajua kabisa halmashauri ni wajanja sana na wanataka kutunyang’anya mashamba yetu ili wawapatie matajiri na sisi tuwe masikini hatutaki kijiji hichi kiwe mji,” alisema Sofia Njau.

Njau alisema wanafurahia kijiji hicho kiwe mji lakini kutokana mashamba walio kuwa nayo ndio wanayotumia kwa ajili ya kilimo na kwamba kilimo hicho ndicho kinachosomesha watoto na mahitaji mengine.

Kwa upande wake afisa mipango wa mji wa halmashauri ya Moshi, Aisha Masanja, alisema lengo la kikao hicho kilikuwa ni wananchi kutoa baraka zao ili waendele na ramani ya mipango miji ya kijiji cha uchira ili kijiji hicho kiwa mji mdogo hali ambayo itafanya wananchi wapate makazi yanayoridhisha na kupitika kwa urahisi.

Masanja alisema wananchi hawakuafiki na kwamba wamekataa kijiji hicho kiwe mji hili iyopeleka kushindwa kuelewa na kuvunjika kwa mkutano huo bila kufikia muafaka.

“Mimi nilivyo waelewa wananchi hawana elimu ya maswala ya mpango miji kinachohitajika ni wananchi wapatiwe elimu ya mipango mji na faida zake naona baada ya hapo ndipo tuanze kazi kupanga huu mji,” alisema masanja.

Alisema wananchi wamejijengea hofu ya kunyanganywa mashamba yao endapo kijiji hicho kikiwa mji kituambao sio cha kweli, kijiji hicho kinaweza kuwa mji na wananchi wakaendelea na kilimo kama kawaida.