Wananchi Waipongeza Proin Promotions Ltd Kupitia Tanzania Movie Talents

Washiriki wa Shindano la Tanzania Movie Talents ambao ni babu na mjukuu wake kiuhalisia wakipongezana mara baada ya kufanikiwa kuingia hatua ya tatu ya kutafuta washiriki 15 bora na hatimaye kupatikana washindi watatu bora wa kanda ya kati ambapo kila mmoja ataondoka na kitita cha shilingi laki tano za Kitanzania.
Mmoja wa washiriki wa shindano la Tanzania Movie Talents akihojiwa na Msanii Joti mara baada ya kufanikiwa kuingia hatua ya tatu hapo kesho huku mjukuu wake pia akifanikiwa kuingia hatua hiyo pia.
Washiriki wa Shindano la kusaka vipaji vya Uigizaji Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents wakiwa kwenye mazoezi wakati walipokabidhiwa muswada (script) kwaajili ya kuifanyia mazoezi na kwenda kuonyesha uwezo wao kwa majaji.
Mshiriki namba 00554 akihojiwa na msanii Joti mara baada ya kufanikiwa kuingia hatua ya tatu hapo kesho ambapo watapatikana washindi kumi na tano bora na hatimaye kupata washindi watatu bora wa kanda ya kati ambapo kila mmoja atajinyakulia kitita cha shilingi laki tano za kitanzania.
 
Baadhi ya washiriki wa shindano la Tanzania Movie Talents wakibadilishana mawazo mara baada ya kupatikana kwa washiriki 30 ambao wataendelea na mashindano hapo kesho kwaajili ya kupata washiriki 15 bora.
 Mmoja wa washiriki wa shindano la Tanzania Movie Talents akiwa amenyongonyea mara baada ya safari yake katika mashindano kuishia njiani kutokana na kukosa nafasi ya kuingia katika hatua ya tatu hapo kesho.Picha na Josephat Lukaza wa Proin Promotions – Dodoma

Na Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited – Dodoma

 Shindano la Tanzania Movie Talents limeingia ya hatua ya pili ya mchujo ambapo washiriki 30 wameweza kupatikana kwaajili ya kuendelea na shindano hilo hapo kesho ambapo washiriki 15 ndio watachukuliwa kwaajili ya kuendelea na mashindano hayo na hatimaye kupatika washindi watatu bora ambao watawakilisha kanda ya Kati na kwa kila mshindi mmoja kuibuka na kitita cha shilingi laki tano (500,000/=).

Mpaka sasa washiriki 30 wameshapatikana kwa kanda ya Kati na hatimaye kesho washindi watatu watapatikana na kuiwakilisha kanda ya Kati katika fainali kubwa itakayofanyika Mkoani Dar Es Salaam na hatimaye mshindi katika fainali hiyo kujinyakulia kitita cha Shilingi Milioni 50 za kitanzania (50,000,000/=)

Katika Washindi 30 waliopatikana leo, washiriki wawili wameweza kuonyesha vipaji vyao huku washiriki hao wakiwa ni ndugu kabisa, washiriki hao ni babu na mjukuu wake wa kike ambao wameweza kufanikiwa kuingia hatua ya tatu kesho ambapo washindi wa Kanda ya Kati watapatikana.

Shindano la Tanzania Movie Talents linatarajiwa kumalizika kesho Kanda ya Kati Mkoani Dodoma na hatimaye kuhamia Kanda ya Juu Kusini ambapo usaili utafanyika Mkoani Mbeya na usaili wa Kanda ya Juu Kusini utaanza tarehe 19 April 2014 saa 1 asubuhi na wakazi wa Kanda ya Juu Kusini wanaombwa kujitokeza kwa wingi ili kuweza kuonyesha vipaji vyao na kuweza kuitumia fursa hii, Vilevile fomu za usaili zitapatikana Siku hiyohiyo ya usaili na fomu hizo hazina gharama yoyote ile.
  
Na Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited – Dodoma
Watanzania wa Mikoa ya Mwanza na Dodoma wameipongeza kampuni ya Proin Promotions Limited kupitia shindano lao la Kusaka vipaji vya Kuigiza Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents kwa kuamua kuanzisha shindano hilo ambalo limeanza kuonyesha matumaini kwa vijana wenye vipaji vya kuigiza ambao walisahaulika katika tasnia hiyo ya filamu nchini.

 

Shindano hili la Tanzania Movie Talents linawawezesha watanzania wote wenye vipaji vya kuigiza kuweza kujitokeza ili kuweza kuonyesha vipaji vyao na kuvikuza kwa kutumia fursa hii iliyoanzishwa na kampuni ya Proin Promotions Limited

 


Wakiongelea kuhusu shindano hili la Tanzania Movie Talents, wakazi wa Mkoa wa Dodoma walisema” tunafurahishwa sana na shindano hili kuweza kuanzishwa Tanzania na Afrika Mashariki na Kati kwani sasa tunaweza kupata nafasi katika tasnia ya filamu baada ya kuanza kuonyesha vipaji vyetu vya kuigiza”

 

“Tanzania Movie Talents inamgusa kila mtanzania mwenye vipaji vya kuigiza kwani ni nafasi kwa vijana na watanzania wote wenye vipaji vya kuigiza kuweza kujitokeza kwaajili ya kuonyesha uwezo na vipaji vyao vya kuigiza, Shindano la Tanzania Movie Talents ni mkombozi wa Vijana na watanzania ambao wana vipaji vya kuigiza ambapo kupitia shindano hili vijana wanaweza kupata nafasi za ajira kupitia tasnia ya filamu nchini ambapo washiriki watakuwa wameweza kuonekana na hatimaye kuitwa kwaajili ya kufanya kazi.

 


Kwa upande wake baadhi ya wafanyakazi wa timu ya Tanzania Movie Talents walithibitisha kuwa ‘Tanzania Movie Talents imepokelewa vizuri na watanzania wa Mikoa ya Mwanza na Dodoma  kwani tumeona ongezeko la washiriki waliojitokeza kwaajili ya usaili wa kushiriki katika Shindano hili kubwa na la kwanza Afrika Mashariki na Kati. Hii nikutokana na ukweli kwamba washiriki wote wanaofika kwaajili ya Usaili hawatozwi kiasi chochote cha pesa kutoka timu ya Tanzania Movie Talents na pia kufurahishwa na uamuzi wa Majaji wa Timu ya Tanzania Movie Talents,  niwazi kabisa kuwa kutotozwa kwa kiasi chochote cha pesa kwa washiriki kumekuwa ni kivutio kikubwa kabisa hivyo kuongeza idadi ya washiriki katika kila Kanda tunayoenda”alisema Stephen Mapunda Mkazi wa Mkoa wa Dodoma