WANAMGAMBO wa kisomali wamewauawa kwa kuwapiga risasi polisi wanne wa Kenya karibu na mpaka wa Somalia, maofisa wamesema. Takriban watu 40 waliojihami kwa silaha walishambulia kituo cha Polisi juzi, kamishna wa kaunti hiyo amesema.
Kundi la alshabaab limethibitisha kufanya shambulio hilo. Kenya imekumbwa na msururu wa mashambulio tangu majeshi yake yaingie kusini mwa Somalia kukabili wapiganaji wa Alshabaab mwaka wa 2011.
Kamishna wa Kaunti hiyo Rashid Khattor ameambia wanahabari: “maofisa wanne wa polisi wameuawakatika shambulio hilo na tunajiandaa kusafirisha miili yao kutoka eneo hilo.
Eneo hilo karibu na Garissa limekuwa likipata mashambulio ya mara kwa mara katika miezi chache iliyopita. Watu 8 waliuawa katika shambulio mwezi Aprili na wengine watano mnamo mwezi Januari.
-BBC