Wanakijiji Kilombero Kumburuza Mwekezaji Mahakamani

Mkazi wa Kijiji cha Chiwachiwa, Comrade Mlonganile (kulia), akizungumza katika mkutano huio wakati akichangia jambo. Kushoto ni Zabron Mpwage mmoja wa wanakijiji hicho.

Mkazi wa Kijiji cha Chiwachiwa, Comrade Mlonganile (kulia), akizungumza katika mkutano huio wakati akichangia jambo. Kushoto ni Zabron Mpwage mmoja wa wanakijiji hicho.

 Mwangalizi wa LHRC, Wilaya ya Kilombero, Godfrey Lwena (kushoto), akizungumza katika mkutano huo kuhusu mgogoro wa ardhi dhidi mwekezaji wa Kampuni ya Usafirishaji ya Union ambaye anadaiwa kuchukuwa ardhi yao ambapo kesho wanakusudia kufungua kesi Mahakama ya Ardhi dhidi yake kwa msaada wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC). Kulia ni mkazi wa kijiji hicho, Jimmy Mwasenga. 
 Mkazi wa Kijiji cha Chiwachiwa kilichopo Tarafa Mgeta Kata ya Mbingu Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro, Merkizedek Mazani (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu mgogoro wa ardhi dhidi mwekezaji wa Kampuni ya Usafirishaji ya Union ambaye anadaiwa kuchukuwa ardhi yao ambapo kesho wanakusudia kufungua kesi Mahakama ya Ardhi dhidi yake kwa msaada wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC). Kulia ni mkazi wa kijiji hicho, Jimmy Mwasenga na Mwangalizi wa LHRC, Wilaya ya Kilombero, Godfrey Lwena.
  Mkazi wa Kijiji  hicho, Jimmy Mwasenga (kulia), akichangia jambo.
Wawakilishi wa kijiji hicho wakiwa kwenye mkutano huo. Kutoka kushoto ni Zabron Mpwage, Comrade Mlonganile, Raina Ngapya, Mwangalizi wa Haki za Binadamu LHRC Wilaya ya Kilombero, Godfrey Lwena, Merkizedek Mazani na Jimmy Mwasenga.
 
WANANCHI wa Kijiji cha Chiwachiwa kilichopo Tarafa Mgeta Kata ya Mbingu Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro kesho wanakusudia kufungua kesi Mahakama ya Ardhi dhidi ya Kampuni ya Usafirishaji ya Union kwa madai ya kuchukua ardhi yao kesi ambayo itasimamiwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).
 
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mwangalizi wa Haki za Binadamu wa LHRC, Godfrey Lwena alisema kesi hiyo wanatarajia kuifunga kesho baada ya kupokea malalamiko ya wanakijiji hicho.
 
“Baada ya kupokea malalamiko ya wanakijiji hicho chenye kaya 850 tulikwenda Halmshauri ya Wilaya ya Kilombero kujua  mmiliki halali wa maeneo ya kijiji hicho ambapo uongozi wa wilaya hiyo ulishindwa kutoa vielelezo vinavyoonesha umiliki halali wa mwekezaji huyo.
 
 
Mkazi wa kijiji hicho Merkizedek Mazani alisema wameanza kuishi eneo hilo tangu miaka 1974 na hawakuwahi kumuona mwekezaji yeyote wanashangaa wanapoambiwa eneo la kijiji hicho ni mali ya mwekezaji huyo hivyo waondoke.
 
Aliongeza kuwa katika kijiji hicho kunamiundombinu ya barabara, shule ya msingi ambayo imesajiliwa kwa namba MG/05/021/142 na kuwa na kijiji hicho kilitangwazwa na Serikali kuwa kijiji kwa tangazo namba 180/2010.
 
Aliongeza kuwa hivi sasa katika kijiji hicho hakuna shughuli zozote za serikali zinazo fanyika kwa kuwa hawakufanya uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa kutokana na mgogoro huo.
 
Mazani alisema kwa mihula mitatu walifanya uchaguzi wa viongozi wao bila ya kuwa na zuio lolote lakini wanashangaa kuzuiliwa kufanya uchaguzi huo kwa barua yenye kumbukumbu namba KDC/E.30/5/VOL.VI/24 kutoka ofisi ya mkurugenzi wa wilaya hiyo wakidai kijiji hicho kutotambuliwa.
 
Mkurugenzi wa Halmshauri hiyo, Anzimina Mbilinyi alipopigiwa simu jana ilikutaka kutoa ufafanuzi wa madai hayo alituma ujumbe mfupi wa simu yake ya mkono kuwa hakuwa katika nafasi nzuri ya kuongea na simu.
 
Mkuu wa Wilaya hiyo, Hassan Masalla alisema anaomba apate muda wa kuwasiliana na wenzake ili apate majibu ya uhakika ya kujibu kwani halikuwa hajui chochote kuhusu madai hayo.
 
Hata hivyo jitihada za kumpata mwekezaji huyo ili kuzungumzia suala hilo hazikufanikiwa. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)