Wanakijiji Kakola Waudai Fidia Mgogi wa Bulyanhulu

Mwenyekiti wa Kijiji cha Kakola, wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga, Emmanuel Bombeda, akiongoza kongamano la wananchi wa kijiji hicho lililokuwa na ajenda ya kutoka na maazimio ya kudai fidia zao kutoka mgogi wa Bulyanhulu.

WAKAZI wa Kijiji cha Kakola, Kata ya Bulyanhulu, Wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga wameazimia kufanya maandamano yasiyo na ukomo kushinikiza mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu kuwalipa fidia zao. Wakizungumza kwenye kongamano la Kijiji hicho lililofanyika jana juni 20,2017, wakazi hao wamepanga kupeleka kero zao Jijini Dar es salaam kwa Rais John Pombe Magufuli pamoja na kufanya maandamano ya kufunga barabara kushinikiza kulipwa fidia zao.

“Kongamano la leo ni kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli kwa kugundua kwamba tulikuwa tunaibiwa kwa muda mrefu. Tangu mwaka 1996 mpaka leo sisi tumeibiwa tu, hatujapata haki hata moja. Hakuna huduma za jamii zinazotambulika ambazo zimefanywa na mgodi”. Alisema mchimbaji mdogo Aziz Mbaga.

Mjumbe wa serikali ya Kijiji cha Bulyanhulu, Mhidini Mfwanguro alisema maazimio ya wananchi wa Kijiji hicho ni fidia kwa wafukiwa na waathirika wa Bulyanhulu mwaka 1996 pamoja na waathirika wengine wakiwemo wafanyakazi waliochishwa kazi kwa kuumia kazini bila kulipwa na kwamba watawasilisha madai hayo kwa wamiliki wa mgodi huo, kampuni ya Barrick Gold Mine.

Mwenyekiti wa kijiji cha Kakola, Emmanuel Bombeda amesema kijiji hicho kilikuwa na vitongoji tisa lakini vitongoji vinne vilichukuliwa na mgodi wa Bulyanhulu bila wananchi kulipwa fidia huku nyumba zao zikibomolewa.

“Tunataka maandamano ya kufunga barabara tulipwe, siwezi kufanya maandamano halafu tusambae, nataka maandamano kama tuliyofanya umeme ukaletwa kijiji cha Kakola, maandamano kama yale ya Musoma ya kupigwa mabomu lakini tulipwe”. Alisema Bombeda.

Diwani wa Kata ya Bulyanhulu, John Kiganga alikiri wananchi wengi kukosa stahiki zao baada ya kuondolewa kwenye maeneo yao ili kupisha uwekezaji wa mgodi wa Bulyanhulu na kusisita kwamba wanapaswa kulipwa fidia zao maana fomu za tathimini zipo na kwamba hata wale waliolipwa fidia, walilipwa kinyume na tathimini ambapo mmoja wa wananchi aliyepaswa kulipwa shilingi milioni 375 alilipwa shilingi laki tano.

Wananchi wa Kijiji cha Kakola wanalalamika kutolipwa fidia zao baada ya maeneo na makazi yao kuchukuliwa na mgodi wa Bulyanhulu, wengine ndugu zao kufukiwa kwenye mashimo, waliokuwa wafanyakazi wa mgodi huo kutaka stahiki zao baada ya kuumia kazini na kuachishwa kazi pamoja na kutaka huduma bora za kijamii ikiwemo barabara za lami na vituo vya afya/hospitali kutokana na uwepo wa mgodi.

 

Diwani wa Kata ya Bulyanhulu, John Kiganga, akizungumza kwenye kongamano hilo

 

Mkazi wa Kakola, Erasto Mapato, akizungumza kwenye kongamano hilo.

 

Mjumbe serikali ya Kijiji cha Kakola, Jedidiah Kitundu, akizungumza kwenye kongamano hilo.

 

Mkazi wa Kakola, John Mutemankamba, akizungumza kwenye kongamano hilo

 

Mchimbaji mdogo wa dhahabu, Aziz Mbaga, akizungumza kwenye kongamano hilo.

 

Mkazi wa Kakola, Erasto Mapato, akizungumza kwenye kongamano hilo.

 

Mkazi wa Bulyanhulu, Waziri Bakari, akizungumza kwenye kongamano hilo.

 

Mkazi wa Bulyanhulu, akizungumza kwenye kongamano hilo.

 

Mkazi wa Bulyanhulu akizungumza kwenye kongamano hilo.

 

Mzee Nikodemas Mabe ambaye ni Mwenyekiti wa wachimbaji wadogo Bulyanhulu akielezea kero zao.

 

Magdalena Lusana akielezea kero za Bulyanhulu.

 

Mzee Geremiah Wangaluke akielezea kero za Bulyanhulu.

 

Kijana Masumbuko Kafula mkazi wa Bulyanhulu akieleza madhira waliyoyapata kutokana na wawekezaji.

 

Mama Melania Baesi akieleza juu ya wanae kupoteza maisha kwenye sakata la Bulyanhulu.

 

Wakazi wa Bulyanhulu wilayani Msalala.

 

Wakazi wa Bulyanhulu wilayani Msalala

 

Kongamano la wananchi wa kijiji cha Kakola lililokuwa na ajenda ya kutoka na maazimio ya kudai fidia zao kutoka mgogi wa Bulyanhulu.