Wanakijiji Hanga waacha kuzalisha tumbaku, sasa walima alizeti na mhogo

Pichani ni wadau na waratibu wa MUVI, Ruvuma.

MUUNGANISHO wa Ujasiriamali Vijijini (MUVI), Ruvuma umefanikiwa kuwavutia zaidi wajasiriamali wa zao la alizeti na mhogo katika Kijiji cha Hanga kilichopo Wilaya ya Namtumbo Mkoa wa Ruvuma.

Ni muda wa saa mbili (kilometa 42) toka Manispaa ya Songea hadi Hanga wanapopatikana wana vikundi wa MUVI, ambao ni makundi ya Amka na Lichipi. Naweza kusema MUVI safari hii imekwenda kivingine zaidi katika kuhakikisha mawasiliano kwa vitendo yanafanikiwa.

Wanavikundi wapatao 50 walihudhuria katika mkutano huo ulioandaliwa na kipengele cha habari awali akizungumza na wana vikundi hao, Dunstan Mhilu aliwataka wana vikundi hao kutumia Radio Jogoo na kuipa Ushirikiano katika katika kuandaa vipindi vyenye ubora.

Muungano wa Lichipi na Hanga ulifanyika Mai 6, 2011, Mwenyekiti wa Amka, Stephano Komba akieleza historia ya kikundi cha Muungano Hanga amesema kulikuwa na sababu ya vikundi hivyo kuungana moja ya sababu hizo ni ujio wa MUVI katika eneo la Hanga.

“Tumeona ni vema kuungana na wana Lichipi kutokana na kubadirishana uzoefu mara kwa mara hua tunaenda kuangalia wanavyo andaa na kupanda alizeti na wao vivyo hivyo. Baada ya hapo MUVI ikatuletea mashine ya kukamua alizeti.

Akiongeza mwenyekiti huyo alisema kwakuwa MUVI huwezesha kwa aslimia kadhaa hususani katka maeneo ambayo kuna upungufu na uhitaji fulani, ndipo wana vikundi walipo anza kuchangishana sh 3000/= kwa kila mwana kikundi kwa ajili ya shimo la mashine hiyo baada ya hapo wakachangishana sh 5000/=

Akizungumza kwa hamasa ya hali ya juu, Cesilia Nyoni alinukuliwa akisema kuwa; “tunaisubiri mashine hiyo kwa hamu mana ikija hata utapia mlo utakwisha badala ya kulanguliwa na kuuza kwa jumla (sadolini) tuta kamua mafuta wenyewe na kuimarisha maisha yetu huo ndiyo mnyororo wa thamani jamani.”

Aidha wameishukuru MUVI kwakuwaongezea nguvu ikiwemo kipengele cha mawasiliano kwa vitendo ambapo hupata elimu kwa vipeperushi, majarida na sasa redio. Philo Lwambano ni mwenyekiti wa Lichipi anasema Radio Jogoo wataitumia ipasavyo kupaisha sauti zao kwani walikuwa wakitamani kuwa na chombo cha kupashana habari kwa mda mrefu lakini wakati ulikuwa haujafika.

“Tunaishukuru MUVI hadi kurekodi vipindi leo hi tumefarijika sana tunaomba muendelee kutuwezesha kwa hali na mali ili tujikwamue kiuchumi juhudi zenu tunaziona hivi karibuni wamekuja watu wa Uyole toka Mbeya na kutupatia mafunzo, leo kipengele cha habari ni jambo muhimu na lakutia moyo.

Naye Afisa Habari wa mradi wa MUVI Bw Dunstan Mhilu amesema zoezi lakurekodi vipindi ni endelevu kwa vikundi vilivyo kwenye mradi wa MUVI mkoa wa Ruvuma na kuwataka waoneshe ushirikiano ili kutimiza malengo yaliyo kusudiwa.

“Wana hanga hamna budi kuitumia redio hii ili kupata elimu na habari mbali mbali kutoka kwa wana vikundi vingine,kwakusikiliza redio Jogoo hususani vipindi vya mradi wa MUVI kutawasaidia kujua ni wapi mmekosea na wenzenu wamefanikiwa kwa namna gani.

MUVI imekijengea uwezo redio Jogoo ili wana vikundi wa MUVI wapate elimu stahiki ya kilimo bora kinacho shabihana na kilimo cha kibiashara kwa kuendeleza mnyororo wa thamani na kuongeza thamani ya bidhaa.

Mwaka huu kila mwana kikundi atalima heka moja ya alizeti na naya mhogo lakini wale wenye nguvu wanaweza kulima hekari nyingi zaidi Bw Christopher Nindi mwana kikundi amesema MUVI iwasadie zaidi kuwa na maafisa ugani wa wilaya,kata,na vijiji ili kuwasaidia .

Mwaka 2010 walichelewa kutokana na pembejeo kuchelewa lakini mwaka huu wameanza maendalizi mapema hivyo kuiomba MUVI kuwafikishia mbegu kwa wakati.

Changamoto waliyo nayo kubwa ni kupambana na pembejeo bado kwao ni tatizo aridhi nyingine haihitaji mbolea lakini nyingine huhitaji mbolea.