Wanajeshi Wanne wa Marekani Wauwawa, 40 Walipuliwa Nigeria

Rais wa Marekani, Barrack Obama

Rais wa Marekani, Barrack Obama


MTU mwenye silaha amewaua askari wanne wa Jeshi la Majini la Marekani katika shambulio lililofanywa kwenye majengo mawili ya jeshi hilo katika Mji wa Chattanooga, Tennessee. Wanajeshi hao wote waliuawa katika jengo moja. Maofisa nchini humo wameyaita mauaji hayo kuwa ni Shambulio la ndani. Shirika la Upelelezi la Marekani FBI linalochunguza mauaji hayo, limesema halijajua bado kilichosababisha shambulio hilo.

Kufuatia tukio hilo maeneo kadhaa yamefungwa zikiwamo hospitali na shule ili kuchukua tahadhari. “Ni mazingira ya kusikitisha kwa watu ambao wametumikia taifa kwa moyo wote, kuuawa katika mfumo huu inasikitisha. Wakati maandalizi ya mawasiliano na familia za wanajeshi hawa yakifanyika, naomba wafahamu kuwa nazungumza kwa niaba ya raia wote wa Marakani kuelezea masikitiko yangu na kuwahakikishia kuwa tupo nao katika mazingira haya magumu”.

Naye Meya wa Jiji la Chattanooga Andy Berke alisema muuaji aliuawa na polisi. Pia ofisa wa polisi pamoja na watu wengine wamejeruhiwa. “tunafahamu kuwa kuna watu wanne waliouawa. Tunafahamu kuwa muuaji pia aliuawa katika eneo la tukio na pia afisa wa polisi mmoja wa Chattanooga amepigwa risasi kwenye kifundo cha mguu na anatibiwa vilevile pale Arlanga, pia kulikuwa na watu wengine waliopigwa risasi na wametibiwa.

Mwanasheria Mkuu wa Jimbo la Tennessee, Bill Kilden, ameyaelezea mauaji hayo kama ugaidi wa ndani.

Wakati huo huo, Wafanyakazi wa kikosi cha uokoaji nchini Nigeria wanasema katika eno la Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo kwenye Mji wa Gombe watu 40 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa baada ya milipuko kutokea kwenye soko katika eneo hilo.

Mlipuko wa kwanza umetokea jirani na eneo la maegesho nje ya duka la viatu, na kufuatiwa na mlipuko mwingine muda mfupi baadae. Mmoja ya wafanyakazi wa uokoaji miongoni mwa waliouwa ni wanawake na watoto. Mashuhuda wa tukio hilo amesema hali ni mbaya kwenye mitaa ya Gombe.

“Tulikuwa hapa sokoni na mara tukaona ndege inapaa angani na baadae ikapotolea mbali, ndani ya dakika tano tukasikia mlio mkubwa wa mlipuko. Tuliona watu wakilipuka kama matairi. Watu wengi walidhani ni matairi yamepasuka, na baadae sekunde chake tukawaona watu wameanguka chini wakiwa wameungua na kuanza kukimbia. Kulikuwa na mlipuko mwingine ambao nao umeua watu wengine. Tulijipa ujasiri na kuanza kuwaondoa watu na kuwapeleka hosptalini.” Alisema Awalu Yakubu.

Na shuhuda mwingine anasema alishuhudi vipande vya miili ya binadamu. “Kulikkuwa na vipande miiili ya binadamu kila mahali wakati tulipokuwa tukiwasaidia waliokuwa wamejeruhiwa. Mtu aliyeuawa kwenye duka lake aliwekwa kwenye begi, kumburutwa barabarani na kupakiwa kwenye gari. Na baadae majeruhi wakasafirishwa.” Amesema shuhuda mwingine Haruna Abubakar.