Wanajeshi wamshambulia kamanda Nigeria

Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan

Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan

WANAJESHI nchini Nigeria, wamemfyatulia risasi Kamanda wao Mkuu katika Mji wa Maiduguri Kaskazini Mashariki mwa nchi. Hata hivyo Meja Jenerali, Ahmed Mohammed alinusurika na kifo hicho. Shambulizi hilo lilifanywa kwenye gari lake katika kambi ya Jeshi ya Maimalari.

Taarifa zaidi zinasema wanajeshi hao walifanya hivyo kwa kile kumlaumu kamanda huyo kwa mauaji ya wanajeshi wenzao walioshambuliwa na kundi la Boko Haram na kuuawa. Wakati huohuo, Rais wa Goodluck Jonathan amesema hayuko tayari kubadilishana wasichana miambili waliotekwa nyara na wapiganaji wa Boko Haram wanaozuiliwa katika magereza ya Nigeria.

Waziri wa Serikali awali alisema kuwa maofisa wa utawala walikuwa tayari kwa mazungumzo na Boko Haram lakini Rais Goodluck Jonathan amesisitiza kwamba suala hilo halitazungumziwa. “Alisisitiza kwamba hataongea na Boko Haram kuhusu kubadilishana wasichana waliotekwa na wapiganaji wa kundi hilo wanaozuiliwa nchini humo,” alisema mwakilishi wa serikali ya Uingereza Mark Simmonds baada ya kukutana na Rais Jonathan kujadili namna ya kuwanusuru wasichana hao.

Hatua ya kutekwa nyara kwa wasichana hao katika Jimbo la Borno Aprili 14, 2014 imesababisha kero kubwa kwa jamii ya kimataifa kiasi cha kulazimisha baadhi ya nchi za kutoa wataalamu kusaidia serikali ya Nigeria kuwatafuta wasichana hao.

-BBC