Wanajeshi wa Marekani waondoka Iraq

Majeshi ya Marekani nchini Iraq

RAIS wa Marekani Barack Obama maeadhimisha kumalizika kwa vita vya Iraq kwa kupongeza “mafanikio yasiyo ya kawaida” kwa vikosi vya Marekani katika mapigano ambayo yalipingwa na wengi.

Katika hotuba yake kwenye eneo la Fort Bragg mjini Carolina Kaskazini, aliwapongeza wanajeshi wale waliohudumu na hata kufariki dunia wakiwa vitani, pamoja na jamii zao. Wanajeshi wa Marekani wa mwisho kutoka nchini Iraq wanatarajiwa kuondoka siku chache zijazo.

Hata hivyo, Wajumbe wa Chama cha Republican wamekosoa mpango huo wa kuondoa wanajeshi Iraq wakielezea wasiwasi uliopo kuhusu usalama wa taifa hilo, lakini raia wengi wa Marekani wanaunga mkono hatau hiyo.

Katika hotuba ya Jumatano, Rais Obama – ambaye kwa kiasi fulani alifanikiwa kuwa rais kwa msimamo wake wa kupinga vita vya Iraq – alipongeza ujasiri wa majeshi ya Marekani katika muda wa miaka takriban tisa kwenye vita hivyo.
-BBC